Jumatano, 14 Januari 2015

KUMBE MTOTO WA CHRISTIAN RONALDO NI SHABIKI WA LIONEL MESSI

cristiano-ronaldo-son-cristiano-junior-in-2013
Katika miaka takribani 10 iliyopita ulimwengu wa soka umetawaliwa na upinzani wa jadi katika ya wanasoka wawili bora kabisa katika kizazi hiki, Mreno Cristiano Ronaldo naLionel Messi.
Lakini pamoja na upinzani walionao uwanjani, wanasoka hao wawili wameonyesha kuwa na uhusiano mzuri wanapokuwa nje ya uwanja, kwa pamoja wawili hao walionyesha hilo wakati walipokuwa Uswisi mwanzoni mwa wiki hii kwenye sherehe za utoaji tuzo yaBallon d’Or.
Katika kuonyesha hawana uadui, imetolewa video inayomuonyesha Cristiano Ronaldo akimwambia Lionel Messi kwamba mwanae ambaye ni Cristiano JR ni shabiki wake mkubwa.
Alikaririwa akimwambia: “Mwanangu anakupenda sana, muda wote anaangalia video zako kwenye mtandao wa intaneti“– Cristiano Ronaldo.
Angalia video yenyewe hapo chini

Share:

0 maoni:

MATUKIO YA VIDEO

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text