
Balotelli ambaye kwa sasa yupo nchini
Marekani akijiandaa na msimu mpya kwa pamoja na wachezaji wenzie wa
klabu ya AC Milan, jana wakiwa kwenye mechi ya pre season dhidi ya
Manchester City, Balotelli akafanya kituko kingine kilichowaacha watu
midomo wazi.
Wakati mchezo ukiwa unaendelea mashabiki
wawili wa AC Milan waliingia uwanjani na kwenda moja kwa moja kumvamia
Mario Balotelli, huku walinzi wakiwa wanawakimbiza kwa nyuma, mashabiki
hao wawili walitoa simu na kumuomba Balotelli kupiga nae picha.
Balotelli alionyesha kufurahishwa na hilo
suala na kutoa ushirikiano kwa mashabiki hao kwa kupozi nao na kupiga
‘selfie’ – kitendo ambacho kiliibua shangwe za kutosha kutoka mashabiki
wengine waliojazana kwenye uwanja wa Pittsburgh.
Mchezo huo uliisha kwa Manchester City kuifunga AC Milan 5-1.
0 maoni:
Chapisha Maoni