Alhamisi, 9 Aprili 2015

BAADA YA AJALI YA TANGA ,HII NYINGINE MOROGORO LEOLEO.....R.I.P KWA WOTE WALIOPOTEZA MAISHA

IMG-20150409-WA0015Mara nyingi stori za aina hii huanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, baadae unaona RADIO na TV nazo zinaanza kuripoti.. Siku ya leo APRIL 9 watu walianza kusambaziana picha za ajali iliyotokea Tanga, mabasi mawili ya abiria na gari dogo yamegongana, watu 10 wamefariki na wengine kujeruhiwa.. kabla siku haijaisha naipokea hii nyingine kutoka Morogoro.
Basi la Kampuni ya Happy Nation lenye namba T 618 BDN lililokuwa likitokea Dar es Salaam kuelekea Mbeya limepata ajali hiyo eneo la Mikumi, Morogoro.. taarifa za awali zinasema watu wawili wamefariki na wengine kujeruhiwa.
IMG-20150409-WA0013

Chanzo cha ajali hakijafahamika, naifuatilia hii kwa ukaribu.. kitakachonifikia nitakusogezea hapa muda wowote mtu wangu.
IMG-20150409-WA0014
IMG-20150409-WA0015
#RIP kwa watu wetu waliofariki kwenye ajali hiyo, pole kwa waliopata majeraha pia.
Share:

0 maoni:

MATUKIO YA VIDEO

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text