Alhamisi, 9 Aprili 2015

Leo kasikika Dayna.. Linex kuhusu video yake kutopigwa MTV na TRACE.. Ngoma mpya ya Young Dee kutoachiwa… #255

trill-entertainment-logo

Jana tumeisikia ngoma mpya ya Dayna Nyange aliyomshirikisha Nay Wa MitegoNitunze’ leo kupitia story za kiburudani zaidi za 255 amezungumzia ishu ya wasanii wa kike kuwashirikisha wasanii wa kiume kwenye ngoma zao.
DSC_1122
Dayna Nyange.
Dayna amesema inategemea na msanii anaimba kitu gani, idea nyingi wanaimba kuhusu mapenzi kwa hiyo wanaamua kuwashirikisha wasanii wa kiume ili kuwakilisha pande zote mbili.
Kumbe Dayna ana list ya wasanii wake anaowaangalia sana kwa sasa.. anayaangalia mafanikio yao pia, yuko DiamondAYOmmy Dimpoz, Nay Wa Mitego… KamtajaVanessa Mdee pia kwa upande wa wasanii wa kike.
d-2Mkali mwingine kwenye 255 ni Linex kulalamikia video yake kukosa airtime kwenye kituoMTV na Trace Tv.. Kasikika tena leo kwenye 255, Linex amesema anachukulia kama changamoto kwa video yake kushindwa kuchezwa kwenye vituo hivyo.. haijamkatisha tamaa, atafanya video nyingine ambayo atahakikisha ina vigezo vya kuchezwa kwenye vituo hivyo.
Kuhusu ishu hiyohiyo ya Linex, Meneja wa Tip Top Connection Babu Tale amesema kukataliwa kwa video hiyo na vituo hivyo ni jambo la kawaida kwa sababu wana vigezo vyao wanavyoangalia kama ilivyo kwa vituo vingine hapa nchini, wakikuta video haina vigezo hivyo hawawezi kuicheza.
babu1-640x360Kuhusu video za Madee, Chege na Temba nazo kutochezwa kwenye vituo hivyo amesema alipeleka ila haikuwa kwenye ukubwa waliokuwa wanautaka.. Tale amesema anategemea kutuma tena kwenye ukubwa wanaoutaka ili zianze kuchezwa.
Young DEE
Rapper Young Dee.
Rapper Young Dee amesema ameshindwa kuachia ngoma yake mpya kama alivyoahidi kutokana na tour yake ya ‘Ongea na Young Dee’ anayoendelea kuifanya kwa kuzunguka mikoa mbalimbali.. kwa sasa anaangalia jinsi ya kukaa na Management yake na kuamua siku ya kuiachia ngoma hiyo.
Bonyeza play kusikiliza story zote za 255 leo…
Share:

0 maoni:

MATUKIO YA VIDEO

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text