Wasanii wazindua kampeni ya kitaifa kuishinikiza serikali kuwatambua katika katiba
Leo asubuhi (February 28) pande za Kinondoni Vijana Social Hall kulikua wasanii wa fani mbalimbali waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya kuzindua kampeni ya kitaifa maalum kwa ajili ya kuishinikiza serikali kuwatambua wasanii kikatiba.
Nikki pia amezungumzia azimio wanalotaka kuliweka
"Tunataka kufanya azimio la kuhakikisha kuwa eidha siku moja au wiki nzima kazi yoyote ya sanaa isiskike kwenye media, Radio Tv magazeti, naposema sanaa kuanzia mziki, katuni, graphics chochote, na kama ni mziki hata mziki wa nje usipigwe maana sisi hapa ni mabalozi wa wasanii wengine duniani, ili watu watambue mchango wa wasanii na watusikilize"