Ijumaa, 28 Februari 2014

Ni juu ya Chelsea kuilinda heshima ya Ligi Kuu ya Uingereza ....!(WWW.SAMERICK.BLOGSPOT.COM)


CHELSEA_51384.jpg
Manchester City 0-2 Barcelona, Arsenal 0-2 Bayern MunichOlympiakos 2-0 Manchester United, Chelsea ?-? Galatasaray.
Haya, mpaka sasa timu zote za Uingeresa zimefungwa magoli mawili kwa bila katika ligi ya mabingwa. Sawa, Arsenal na Man City walifungwa na timu bora Ulaya, lakini, Manchester United kufungwa na Olympiacos ni aibu!
Ndio, Ligi ya Mabingwa ni ligi ya vilabu bora duniani, lakini, dunia ya soka inaamini kwamba Ligi Kuu ya England ni ligi bora duniani.
Ligi Kuu ya England ni ligi bora kwa kuwa kuna timu nyingi nzuri, lakini haimaanishi kwamba vilabu katika ligi hii ni vilabu bora duniani.
Ligi hii ni nzuri kwa sababu hakuna klabu yenye kiwango kikubwa sana kuliko vilabu vingine. Kwa mfano, msimu huu sijapata furaha sana kuangalia ligi ya Ujeruman, ni kwa kuwa Bayern Munich wamefikia kiwango cha kimpira ambapo hakuna timu ambayo inaweza kushindana nao! Nafurahi kwamba hakua timu kama Bayern Munich katika Ligi Kuu ya England, ni kwa kuwa wangefanya kusiwepo na ushindani katika ligi hiyo.
Hata hivyo, bado ni ajabu kwamba hakuna klabu ambayo itawakilisha Ligi Kuu ya England katika hatua ya tatu ya Ligi ya Mabingwa.
Usiku huu Chelsea wanacheza dhidi ya Galatasaray. Ukilinganisha na Arsenal na Man City, Chelsea hawajapata mpinzani mkubwa. Lakini, ikumbukwe kwamba Galatasaray waliwatoa Juventus katika hutua ya kwanza.
Pia shujaa wa zamani wa Chelsea, Didier Drogba anacheza dhidi ya klabu yake ya zamani. Naamini, kwamba mchezaji huyu atafanya kila anachoweza kuifunga timu yake ya zamani. Mwaka 2012 Chelsea ilikuwa timu pekee ya Uingereza ambayo ilifuzu hatua ya tatu ya Ligi ya Mabingwa.
Sitashangaa kama watakuwa timu pekee kutoka Ligi Kuu ya Uingereza kufuzu hatua ya tatu katika msimu huu pia.
Olle,Sweden. (R.M)
Share:

0 maoni:

MATUKIO YA VIDEO

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text