AMUUA MKE WAKE KWA AJILI YA WIVU WA MAPENZI
Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Bwana Ulrich Matei amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amemtaja mwanaume huyo kuwa ni muinjilisti wa kanisa la Agrikana huko kijijini Gama .
Aidha Kamanda Matei amesema siku ya tukio hilo muinjilisti huyo alitoka nyumbani akiwa na mkewe na mtoto wao Sabrina mwenye umri wa miaka 10 na kuelekea porini kwa ajili ya kukata miti ya kuchoma mkaa.
Hata hivo kamanda Matei amesema wakiwa porini walimtuma mtoto wao nyumbani, baada ya mtoto huyo kuondoka ndipo Muinjilisti alichukuwa panga na kumkata mkewe na kisha yeye kujinyonga hadi kufa.
0 maoni:
Chapisha Maoni