
Pichani ni madiwani wa manispaa ya Iringa, waliohudhuria semina iyo iliyofanyika leo katika ukumbi wa Maji-IRUWASA.
Na Riziki Mashaka, Iringa
Semina ya
Madiwani wa Manispaa ya Iringa, wakiendelea na semina inayoendeshwa na
mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Iringa mjini katika ukumbi wa
maji uliopo katika majengo ya ofisi za mamlaka hiyo, madiwani wa
IRUWASA katika manispaa hiyo walihudhuria semina hiyo inayolenga
kuboresha huduma ya maji kwa wakazi wa manispaa hiyo, maudhui ya semina
hiyo ni uhakika wa maji na nishati ili kuimarisha sekta ya maji pia
kutoa huduma bora kwa wakazi wa manispaa ya Iringa.

Diwani mmoja akitoa hoja zake katika mkutano huo.

Mgeni rasmi katika semina hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya IRUWASA, Bw. Muhongole akitoa hoja mbele ya madiwani waliohudhuria semina hiyo.
Semina hiyo iliendeshwa na Eng, Martin Lusindiko ambaye pia ni meneja mtendaji upande wa mitambo ya IRUWASA na mgeni rasmi katika semina hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya IRUWASA, Bw. Muhongole, alihudhuria na kutoa mchango wake katika semina hiyo ya wiki ya maji. Madiwani hao walikaa katika meza moja na kujadili mambo muhimu ili kukuza sekta hiyo kama vile kujadili gharama inayoingia na kutoka kwa kila mwezi, matengenezo ya miundombinu mfano utengenezaji wa mabarabara na mabomba yanayosambaza maji katika maeneo husika ya manispaa hiyo, IRUWASA inatumia huduma ya maji yanayozalishwa na nguvu ya nishati na maeneo ya mwinuko maji usambazwa pia kwa kutegemea nguvu ya nishati.

Bw. M. Lusindiko ndiye aliyekuwa mwendeshaji mkuu wa semina hiyo ambaye pia ni meneja mtendaji upande wa mitambo ya IRUWASA akiwa anatoa ufafanuzi katika semina hiyo.
Madiwani hao walijadili mambo mengi katika mipango mikakati yao ya kuboresha huduma za IRUWASA kama maeneo ya gharama na kuainisha viwango vya pesa vinavyoikabili mamlaka hiyo ; gharama za kuzalisha maji (umeme, dawa, mishahara na mengine), maslahi ya watumishi, utawala, kutangaza biashara na kibenki.

Mkurugenzi mtendaji wa IRUWASA, Bw. Martin Mfugale alipokuwa anajibu baadhi ya maswali ya madiwani katika semina hiyo.
Mamlaka hiyo bado ipo katika mpango mkakati wa kupandisha bili ili kufidia kiasi cha fedha zilizopotea kutokana na gharama zisizokudiwa kama wizi, na upotevu wa matumizi yasiyo sahihi yaliyosababisha matumizi makubwa ya fedha katika sekta hiyo, hivyo EWURA (Consumer Consulatative Council) ndio wenye mamlaka ya kuidhunisha bei hizo, kila diwani alieleza changamoto anazozikabili katika sekta yake na hata kuuliza maswali, kuchangia mawazo na tathmini tofauti kwa lengo la kuimarisha maendele ya sekta hiyo.

Pichani ni viongozi hao wa IRUWASA wakipata chakula, kutoka kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa IRUWASA, Bw. Martin Mfugale, katikati ni mgeni rasmi katika semina hiyo ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya IRUWASA, Bw. Muhongole na meya wa IRUWASA, manispaa ya Iringa.
Katika semina hiyo, Madiwani hao walijadili masuala mengine kama vile bei za maji, utozaji wa bei za maji, upangaji wa bei pia malengo ya bei zinazopangwa na IRUWASA.
Mkurugenzi mtendaji wa IRUWASA, Bw. Martin Mfugale alikuwa akijibu maswali ya madiwani hao ambao walitaka kujua kuhusu msimamo wa mamlaka hiyo katika changamoto zinazotokea, na jinsi watakavyozikabili ili kuinua na kuimarisha sekta hiyo katika manispaa ya Iringa.
Mamlaka hiyo ilitoa zawani nono kwa baadhi ya wahudumu wake ambao ni watuamiaji na walipaji bili bora, washindi walitunukiwa vyeti vya heshimu na kiasi kadhaa cha fedha kwa kila mmoja kama motisha kutokana na mchango wao unaopelekea maendeleo ya mamlaka hiyo pia jamii inayowazunguka, hivyo IRUWASA ina dhamiria kuboresha suala la UHAKIKA WA MAJI NA NISHATI, kauli mbiu inayoenda sambamba na kaulimbiu ya kimataifa (Dunia) ambayo ni WATER AND ENERGY inayotumika kote ulimwenguni.

baadhi ya madiwani wakiwa katika foleni tayari kwa kuchukua chakula

Mmoja kati ya washindi waliozawadiwa katika semina hiyo, Bw. Samweli Kinyunyu akipokea bahasha ya fedha.

Watumishi wa IRUWASA walipopata picha ya pamoja baada ya kusisha zoezi hilo jana.
0 maoni:
Chapisha Maoni