
Polisi
mjini Mombasa wamemkamata mshukiwa wa tatu wa ugaidi na kunasa silaha
zaidi katika gari lililokuwa limebeba mabomu mawili Jumatatu jioni
katika mtaa wa Changamwe.
Mshukiwa
huyo alikamatwa na polisi wa kupambana na ugaidi waliopata taarifa
kutoka katika idara ya ujasusi na mashirika mengine ya usalama.
Inaaminika
kuwa mshukiwa huyo alikuwa kiongozi wa njama ya shambulizi iliyotibuka
na alikuwa ametoroka wakati washukiwa wenzake wawili walipokamatwa
Jumatatu jioni.
Washukiwa waliokamatwa Jumatatu walikuwa wanapanga kufanya mashambulizi katika sehemu ambazo hawakutaja mjini Mombasa.
Walitarajiwa kufikishwa mahakamani Jumanne ingawa polisi waliomba muda zaidi kufanya uchunguzi.
Kwa mujibu wa kamishna mkuu wa Mombasa, wataalamu wa mabomu walitegua mabomu hayo.
Pia
walinasa mitungi sita yenye uzito wa kilo 60 yenye uwezo wa kulipua
majengo, maguruneti sita, bunduki aina ya AK-47 na risasi 270 pamoja na
vifaa vitano vya kulipua mabomu ikiwemo simu ya mkononi.
Maafisa wa ujasusi waliweza kunasa mawasiliano yao na kuweza kuwakamata washukiwa hao.
Mombasa
ni mji unaosifika kwa utalii lakini hivi karibuni umekuwa ukikumbwa na
harakati za vijana wa kiisilamu kukumbatia itikadi kali za kidin
0 maoni:
Chapisha Maoni