Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete
akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani
ya Jimbo la Chalinze leo Machi 18,2014.Katika Mikutano yake kwenye
Vijiji vya Mindukene, Msigi na Kisanga ndani ya Jimbo hilo,Ridhiwani
Kikwete ameahidi kuhakikisha vijiji vyote kwenye jimbo hilo vinakuwa na
matrekta ili kuboresha kilimo.Picha na Othman Michuzi

- Mgombea
Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete
akifurahia jambo na Mzee Joseph January wa Kijiji cha Kisanda,Kata ya
Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze.Picha na Othman Michuzi
MGOMBEA wa Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete ameahidi kuhakikisha vijiji vyote kwenye jimbo hilo vinakuwa na matrekta ili kuboresha kilimo kiwe na tija.
Alitoa ahadi hiyo wakati wa mikutano ya kampeni kwenye vijiji vya Mindukene, Msigi, Kisanga vyote vikiwa kwenye kata ya Talawanda.
"Nikianikiwa kupata ubunge nitahakikisha kila kijiji kinakuwa na matrekta kwa ajili ya kuwa na wakulima ambao wataweza kulima kwa faida kwa ajili ya chakula na ziada kuuza ili kujiongezea kipato," alisema Kikwete.
Akizungumzia changamoto ya migogoro ya wakulima na wafugaji alisema kuwa atahakikisha anazikutanisha pande zote ili kujua chanzo cha migogoro hiyo.
"Tatizo kubwa ni viongozi kushindwa kuzikutanisha pande zinazohusika badala yake wanaongea na upande mmoja jambo ambalo haliwezi kumaliza migogoro hiyo ambapo njia pekee ni kuwa na matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo kwa wakulima na wafugaji," alisema Kikwete.
Aidha alisema kuwa migogoro hiyo inatokana na wafugaji kuingia kinyemela pasipo kufuata taratibu bila ya kupitia kwenye mikutano mikuu ya serikali za vijiji.
Katika hatua nyingine aliwataka wazazi kuepukana na tabia ya kuuza kiholela maeneo yao hali ambayo itasababisha vijana kukosa ardhi kwa ajili ya kilimo na makazi.
Aliongeza kuwa atahakikisha anaboresha masuala mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu, afya, miundombinu, kilimo, mikopo kwa vijana na akinamama, uzinduzi rasmi wa kampeni unatarajiwa kufanyika kesho Aprili huko Chalinze na uchaguzi utafanyika Aprili 6 mwaka huu.
0 maoni:
Chapisha Maoni