Ikiwa
inakaribia wiki ya pili sasa tangu kundi la Sauti Soul kuachia video
ambayo imeleta utata na baadae kutoka taarifa za kufungiwa,hatimae leo
kuna kauli kutoka kwao kama Sauti Soul kuhusu hii video.
Miongoni mwa maoni ya watu kuhusu video hiyo ambayo bado imezua utata
na hisia tofauti ni ile hali ya kuonyesha misuli iliyotajwa na mafans
wa kike kama jambo la kufurahisha huku upande wa kiume wakisema kama
inawadharirisha.

Kwa
mujibu wa bendi nzima la Sauti Soul video ya Nishike ilitungwa tu kwa
ajili ya kutuma ujumbe>>’Tuna pitisha ujumbe kwamba wanaume sharti
wafanye mazoezi sio tu kupata sixpacks lakini kwa ajali ya afya yao’
‘Wengi wetu wamekua wanene kupita kiwango na njia ya pekee ya
kupunguza unene huo nikupitia kufanya mazoezi kwenye gyme’.asema Delvin
Mudig ambaye ni miongoni mwa waimbaji wanaounda Sauti Soul
Katika kauli nyingine Austin Chimano ambaye pia ni member wa Sauti
Soul amesema>>’Hatukukiandaa video ya Nishike kukera mtu yeyote
tunacheza na kuimba Kisauti Soul.tumekua sisi tu.hatukupanga kua na
wimbo ulitakaozua hisia kama hizi Ilikua tu ni dhihirisho la
penzi.hakukua na fumbo hapo’.
Naye Bien Aime Baraza ameongezea>>’kama bendi Sauti Soul sasa
inawekwa kwenye kiwango sawa na bendi za hadhi ya juu kama P-Square,
Mafikizolo,Mikasa na wengine tumekuwa kutoka wakati wa Lazizi na
tungependa mafans wetu waendelee kutusapot kutuwezesha kuwa na
kujulikana nje ya Bara la afrika’
Mwingine ni Polycarp Otieno ambaye yeye amesema>>’Sanaa inahusu
kujieleza na kwetu haikua tu tutoe wimbo ambao watu wangeu skiza na
kuridhika,lakini kitu ambacho kiingeonyesha hilo kwenye video,ndio
tumepata maoni mabaya kutoka kwa wanaume,lakini tunawajibu kua
‘usimchukie mchezaji’, kwa kweli video inayotokea niya kuwahamazisha
watu wafanye zoezi’.