
Toka hii ishu imevuja Stiviano ambae alikua ni ‘nyumba ndogo’ ya Donald amekua akikwepa waandishi wa habari ambapo aliamua kuvaa kifaa maalum kabisa ili kuepuka kuhojiwa na waandishi wa habari.
Mmoja kati ya Wamarekani waliotoa maoni yao kuhusu Stiviano alisema ‘huyu binti anaweza kuwa mpuuzi wa kupindukia… japokua mimi ni Mweusi, sijali kama Donald alikua mbaguzi ama la… msichana kama huyu anawezaje kumsaliti mtu aliempa magari ya kifahari Ferarri, Bentley mbili na nyumba ya kifahari? huyu binti hajatenda haki’

Bilionea wa kimarekani Donald Sterling alikiri kwamba sauti iliyosikika ikitoa maneno ya kibaguzi ni yake hivyo akaadhibiwa kwa kutojihusisha na timu yake milele na kulazimishwa kuiuza timu hiyo.





0 maoni:
Chapisha Maoni