
Uzinduzi
wa chapisho la Tatu la Taarifa za Msingi za Kidemografia, Kijamii na
kiuchumi linalotokana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 (Basic
Demographic and Socio-Economic Profile) katika ngazi ya Taifa uliokuwa
umepangwa kufanyika siku ya Ijumapili tarehe 25 Mei, 2014 umeahirishwa.
Uzinduzi
huo sasa utafanyika rasmi tarehe 10 Juni, 2014 katika ukumbi wa
Kimataifa wa Mikutano wa Mwl. Julius Nyerere uliopo mtaa wa Shaaban
Robert jijini Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 asubuhi.
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mgeni rasmi katika uzinduzi huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Aidha,
uzinduzi huo unatarajiwa kuhudhuriwa na watu wapatao mia tano (500)
ambao ni pamoja na Viongozi mbalimbali wa ngazi za juu Serikalini,
Mabalozi, Wadau wa Maendeleo, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Vyama vya
Siasa, Wawakilishi wa Mashirika yasiyo ya Serikali na Wadau wa Takwimu
nchini.
Kwa
kifupi chapisho hili linatoa viashiria mbalimbali ambavyo ni pamoja na
Kiwango cha uzazi, umri wa kuishi wa mtanzania, vifo vya watoto
wachanga, kiwango cha vifo vya wakina mama vitokanavyo na uzazi na
taarifa nyingine kwa ajili ya kupanga mipango ya maendeleo.
Chapisho
hili ni mwendelezo wa machapisho mbalimbali yanayotolewa na Ofisi zetu
mbili yaani Ofisi ya Taifa ya Takwimu na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa
Serikali, Zanzibar kama ilivyoainishwa kwenye kalenda ya machapisho ya
Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012.
0 maoni:
Chapisha Maoni