
Maafisa
wanaoongoza juhudi za kuitafuta ndege ya Malaysia MH370 iliyopotea ikiwa
njiani kwenda China, wamesema kuwa shughuli ya kuitafuta huenda
ikachukua hadi mwaka mmoja.
Akiongeza
na wandishi wa habari nchini Malaysia, afisa mkuu Angus Houston alisema
kuwa ana Imani kuwa msako wa mwaka mmoja utaweza kutegua kitendawili
cha ndege hiyo.
Maafisa
nchini Australia, China na Malaysia, watakutana mjini Canberra wiki
ijayo, kujadili juhudi za kusaka mabaki ya ndege hiyo ambazo bado
zinaendelea
Mnamo siku ya Alhamisi, kulikuwa na taarifa kwamba ndege ya MH370 ilianza kutafutwa baada ya saa nne za kupotea kwake.
Ripoti ya
hapo awali kutoka kwa waziri wa usafiri wa Malysia, pia ilisema kuwa
wahudumu wa trafiki ya ndege, hawakugundua kuwa ndege hiyo ilitoweka
hadi dakika kumi na saba baada ya kukosa kuonekana katika mtambo wa
Radar.
Ndege hiyo ilikuwa imewabeba watu 239 ilipotoweka ikiwa katika anga ya kusini mwa bahari ya China njiani kuelekea Beijing.CHANZO BBC,(A.I)
0 maoni:
Chapisha Maoni