• This is default featured slide 1 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

  • This is default featured slide 2 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

  • This is default featured slide 3 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

  • This is default featured slide 4 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

  • This is default featured slide 5 title

    Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these sentences with your own descriptions.This theme is Bloggerized by NewBloggerThemes.com.

Jumanne, 22 Aprili 2014

SITTA AIFUATA UKAWA Z'BAR



Dodoma/ Z'bar. Wakati viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiweka kambi Zanzibar, Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta jana naye alitumia siku nzima visiwani humo akikutana na baadhi ya viongozi wa Serikali, katika kile kinachotafsiriwa kuwa kulinusuru Bunge hilo.
Habari zilizolifikia gazeti hili kutoka Zanzibar zinasema Sitta alikutana na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Makamu wa Kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad, Rais Mstaafu, Aman Karume na mwanasiasa wa siku nyingi wa CCM, Mzee Hassan Nassor Moyo.
Zanzibar kwa sasa ndiyo moyo wa upatikanaji wa Katiba Mpya kutokana na wajumbe wake katika Bunge kutegemewa ama kuipitisha au kuikwamisha kwa kuwa kila upande kati ya mbili zinazovutana, hauna uhakika wa kupata theluthi mbili za kura.
Baada ya kuondoka bungeni na kutangaza kususia vikao vya Bunge hilo Aprili 16, mwaka huu, siku mbili baadaye viongozi wa Ukawa waliingia Zanzibar wakitaka kufanya mikutano ya hadhara kuwaeleza wananchi sababu za kufanya hivyo, lakini wakazuiwa na polisi na hadi jana walikuwa wanasubiri kibali. (J M)
Safari ya Sitta
Katibu wa Bunge Maalumu, Yahya Khamis Hamad pamoja na kuthibitisha ziara ya Sitta Zanzibar kuwa alikuwa akutane na Dk Shein, alisema hafahamu lolote kuhusu mkutano wake na Maalim Seif ambaye pia ni Katibu Mkuu wa CUF.
"Sifahamu malengo ya safari wala walichokwenda kuzungumza, ila ni kweli kwamba alifika Zanzibar leo (jana) na alitarajiwa kuondoka jioni kurejea Dodoma," alisema Hamad na kuongeza:
"Hilo la kuonana na Maalim Seif silifahamu ila ninachojua aliniambia nimfanyie miadi ya kuonana na Dk Shein na nikaifanya kama alivyoelekeza."
Mapema habari zilizolifikia gazeti hili kutoka Zanzibar zilisema, Sitta baada ya kukutana na Karume, Shein na Mzee Moyo alitarajiwa kukutana na Maalim Seif saa 9:00 alasiri.
Katibu wa Maalim Seif, Issa Kheri Hussein alithibitisha kwamba Sitta alikutana na kiongozi huyo nyumbani kwake, Mbweni saa 9:30 alasiri jana, lakini alidai kutokuwa na taarifa za mazungumzo hayo.
"Hilo naweza kulithibitisha kwamba mkutano huo umefanyika lakini mazungumzo yenyewe yalikuwa ya faragha na mimi baada ya Sitta kufika niliondoka, hivyo sikuweza kufahamu kilichozungumzwa kwa undani, pengine mpaka nizungumze na Maalim mwenyewe," alisema Hussein.
Ziara ya Sitta kwenda Zanzibar imekuja wakati ambao kumekuwa na wasiwasi mkubwa wa kukwama kwa vikao vya Bunge hilo kutokana na msimamo wa Ukawa.
Share:

JESHI LA OKOA WATU 10

111014220509_sp_joseph_kony_304x171_afp_nocredit_27ed8.jpg

Jeshi la Uganda limesema kuwa limewaokoa watu 10 , saba kati yao wakiwa watoto, waliokuwa wametekwa nyara na wapiganaji wa kundi la waasi la LRA.
Watu hao waliokolewa katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, ambako kundi la LRA limekuwa likiendesha harakati zake kwa miaka mingi.
Msemaji wa jeshi la Uganda, amesema kuwa kamanda mmoja wa kundi hilo Charles Okello, alikamatwa pamoja na wapiganaji wengine wanne.
Marekani imekuwa ikisaidia wanajeshi wa Muungano wa Afrika wanaomsaka kiongozi wa kundi hilo Joseph Kony kwa kuwapa ushauri na kuwasaidia na ndege wanazotumia kumsaka kiongozi huyo.Chanzo BBC, Taarifa na (A.I wa Mjengwa blog)
Wanajeshi hao hawamsaki Kony tu anayetakikana na mahakama ya kimataifa ya jinai ICC, bali wanawatafuta na viongozi wengine wakuu wa kundi hilo
Share:

Jumatano, 16 Aprili 2014

KUTANANA NA AKAPELLA YA OMMY DIMPOZI KAMA MKONGOMANI

Screen Shot 2014-04-16 at 10.32.51 AMKatika kitu ambacho wengi hawafahamu kuhusu mkali huyu anaetoka kwenye mkoa karibu na Congo Ommy Dimpoz, ni ucheshi alionao, ni muongeaji sana ambae mara nyingi ukikaa nae lazima akuchekeshe sana na kuna namna ambavyo anaweza kuibadilisha sauti yake na kuongea kama mtoto aliebanwa na meza, yani ni noma.
April 15 2014 usiku ametoa kali pale ambapo ametoa akapela ya Kikongo kupitia video aliyoipost instagram ambayo iliwagusa wengine kama Ben Pol mpaka wakacomment.
Share:

KIMEWAKA HUKO MJINI DODOMA BUNGENI



SHEKHE wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu amewataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaowakilisha kupitia taasisi zao kwenye mchakato wa kuipata Katiba mpya kutokubali kununuliwa na wawakilishi wa vyama vya siasa.
Alisema hayo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye chakula cha pamoja kati ya watoto yatima na wajane kilichoandaliwa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) kata ya Chang’ombe mjini hapa.
Alisema wajumbe hao wanaotoka uwakilishi wa taasisi mbalimbali ndani ya Bunge hilo wanatakiwa kutoa mawazo ambayo yatanufaisha na kuwagusa Watanzania wote na siyo yenye mtazamo wa itikadi za kichama kama wanavyotaka wanasiasa hao.
Kiongozi huyo wa dini alisema wawakilishi hao wamechaguliwa kwa ajili ya kupendekeza mahitaji yao kwenye katiba hiyo, hivyo wasikubali kununuliwa na vyama vya siasa ambavyo vinataka kuingiza itikadi za kisiasa ndani ya katiba.(Martha Magessa)
Pia amelitaka Bunge hilo kutopoteza muda kwa ajili ya malumbano yasiyokuwa na hoja muhimu ambayo yamekuwa yakiwakera watanzania ambao wanaisubiri Katiba itakayoboresha maisha ya wananchi.
Alisema inasikitisha kuona na kusikia kupitia vyombo vya habari wabunge hao wakichukua muda mwingi, kukashifiana na kulumbana kwani huko ni kupoteza muda huku wajumbe hao wakiendelea kupata posho bila kufikia maamuzi yatakayotengeneza hiyo Katiba.
Awali akisoma risala kwa niaba ya watoto yatima na wajane Mwenyekiti wa Baraza hilo, kata ya Chang’ombe Salumu Mabada, aliwataka wajumbe maalumu wa Bunge la Katiba kuendelea kuhubiri amani na upendo kwa muda wote wanapokuwa ndani na nje ya kikao badala ya kupandikiza chuki na migogoro na hatimaye kuleta mafarakano kwenye mchakato mzima unaoendelea wa kuipata katiba.
Aidha aliwataka wajumbe hao ambao miongoni mwao wanatoka taasisi za kidini, kuendelea kumtanguliza Mungu ili amani itawale na hatima Katiba ipatikane yenye kukubalika na watu wote. 
CHANZO:HABARILEO
Share:

MELI YALETA MAAFA MAKUBWA HUKO KOREA KUSINI NI MELI YA WATU 460 YAZAMA

Ferry yenye abiria 460 ikizama Korea Kusini.

Ferry yenye abiria 460 ikizama Korea Kusini.
Oparesheni ya uokozi inaendelea kufuatia ishara za dharura zilizoripotiwa kutoka meli moja iliyobeba takriban abiria 460 katika pwani ya Korea Kusini.
Maafisa wanasema kuwa walinzi wa pwani hiyo wanatumia, meli za wanamaji wa Korea pamoja na ndege za uokoaji kuwaokoa watu waliokuwa katika meli hiyo.
Shughuli zinaendelea hivi sasa kuokoa zaidi ya abiria 460 wa ferry hiyo .
Jeshi la wanamaji likishirikiana na maafisa wanaolinda usalama katika bahari ya rasi ya Korea wanasema watu wengi wamefanikiwa kuolewa.
Maafisa wanasema walipokea habari kuwa meli hiyo imepata matatizo ikiwa imebeba idadi kubwa ya wanafunzi ikitoka Incheon iliyoko kwenye visiwa vya kifahari vya Jeju .
Waokoaji wamewanusuru tayari abiria 160 huku wengine waliosalia wakishauriwa waruke baharini iliwaokolewe.
Walioshuhudia wanasema kulisikika kishindo kikubwa kabla ya ferry hiyo kuanza kuzama zaidi ya kilomita 20 kutoka ufukweni.CHANZO:BBC(Martha Magessa)
Share:

Kuhusu Post ya Mwana Fa inayomhusu Mrisho Mpoto ‘Mjomba’.

faKupitia ukurasa wa Facebook wa member aliyekua akiwakilisha East Coast Team Mwana Fa amepost picha ya Gari inayomuonyesha Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ akiwa kaegemea gari ya kifahari,bado watu wamekua na maswali kuhusu gari hiyo kama ni ya Mrisho Mpoto.
10255675_10152315259181001_2072835938830301636_nJuu ya maandishi ya post hiyo Mwana Fa aliandika ‘unaleta Mchezo na Mjomba sio’ Bado hakuna jibu la moja kwa moja kuhusu gari hiyo millardayo.com inamtafuta Mrisho Mpoto kupata uhakika wa taarifa hizi ambazo zimesambaa kupitia picha hiyo ya gari aliyoonekana nayo aina ya Toyota Prado New Model rangi nyeusi.
Share:

Alichosema bungeni Mh. Wassira kuhusu Tundu Lissu

Screen Shot 2014-04-16 at 1.04.05 PMApril 16 2014 saa saba kasoro mchana makamu mwenyekiti wa bunge la katiba hapa Dodoma aliwasha kipaza sauti na kuzungumza kuhusu matangazo mawili yaliyomfikia, moja la wageni na la pili ni la hati ya muungano ambayo hatimae imepelekwa bungeni baada ya kuzungumziwa sana na Wajumbe mbalimbali hasa wanaotaka uwepo wa serikali tatu waliosema hati hiyo haipo.
Makamu Mwenyekiti alisema ‘nimepokea hati ya makubaliano ya muungano na ni certified copy na sasa nampa dakika mbili Mh. Wassira atoe maelezo ya hati hii’
Mh Wassira akaanza >>  1. Juzi nilisimama katia bunge hili na kusema kwamba hati ya muungano iliyokua inapigiwa kelele sana, ipo katika hali nzuri na ndani ya siku mbili itafikishwa bungeni.
  1. Sisi wote tumeapa na mwisho wa kiapo chetu tukasema ewe Mungu nisaidie, Mungu wa madhebu yote ni Mungu wa ukweli na uongo ni kazi ya shetani, wamegawana kabisa Mungu wa ukweli na Shetani wa uongo.
  2. Baada ya hati kupatikana jana Tundu Lissu na wenzake wamekutana wakazungumza kwamba sasa tusema sahihi ya Karume sio sawa, tunaipeleka wapi Tanzania? yani kila siku uongo unataka utawale Tanzania na ukweli upuuzwe?
  3. Watanzania tujihadhari sana na Mawakala wa shetani maana Mungu anatumia Wanadamu kufikishia ujumbe wake kwa Wanadamu wengine na Shetani anatumia Wanadamu pia, lazima tukwepe mamlaka ya shetani na Mawakala wao.
  4. Mh. Tundu Lissu amewakashifu waasisi wa taifa Mzee Karume na Mwl. Nyerere Mungu awaweke mahali pema, anasema ni madikteta na waongo…. mimi nasema heshima ya viongozi wetu waasisi hailindwi na vyama, italindwa na Watanzania wote, wajibu wa kulinda heshima yao ni wa wote.
  5. Hatuzuii mtu kusahihisha sera lakini huwezi kusema viongozi wetu wale walikua ni waongo na Madikteta, hatuna haki ya kuwakashifu, namwambia rafiki yangu Tundu Lissu, ulinzi wa heshima ya viongozi hawa ni wa Watanzania na utalindwa kwa gharama yoyote.
Share:

Jumatano, 9 Aprili 2014

NDEGE YA MAAJABU

ndege_9cc12.png
Nchini Kenya kuna Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Naivasha ambae katengeneza ‘Ndege’ yake ambayo toka ameanza kuiunda alisema lazima ipae huku akiwa katumia ( vifaa mbalimbali kutoka kwenye Bajaji kuiunda.
Kazi ilipokamilika nyumbani kwao alipoitengenezea, Polisi wa mji huo wakamkataza kuipaisha kwa sababu ni kinyume na sheria lakini ili kuepuka kumkatisha tamaa… wakamwambia ni vyema akapata kibali kutoka kwa mamlaka ya anga.
Paul Karanja alizuiwa na polisi kuipaisha hii ndege kutoka uwanja wa mdogo wa ndege wa Karagita na kuwanyima uhondo zaidi ya watu 500 waliofika asubuhi ya saa 3 kuangalia chombo kikipaishwa.
njemba_746ec.png
Hata hivyo Mwanachuo huyu wa chuo kikuu cha Meru ana imani ataipaisha ndege yake siku moja ili kutimiza ndoto yake ambayo hata hivyo ilipata hitilafu kwenye uwanja wa ndege wa Karagita kutokana na hali mbaya ya uwanja huu iliyosababisha tairi la ndege yake kuharibika.
Karanja ambae ni Mwalimu pia wa shule ya upili, amesema tayari ameiandikia barua mamlaka ya ndege nchini Kenya kuhusu kupaisha ndege hiyo lakini hajapata majibu.(awadh ibrahim)
Share:

SKYLIGHT WAZINDUA WIMBO WAO MPYA KARIAKOO

skay_be950.jpg
kio_b84da.jpg
Skylight Band ni Bendi ya Muziki wa Kisasa inayomilikiwa na Kampuni ya Skylight Entertainment Limited ambayo ilianzishwa Mwaka mmoja uliopita,aina ya muziki( wa wanaofanya Skylight ni  Afropop ambayo ina mkusanyiko wa ladha za kiafrika..
April 09 2014 wameachia wimbo wao mpya unaoitwa Kariakoo ambapo mbali na kuachia wimbo huu mpya pia wamezindua studio zao za kurekodi muziki zinazoitwa Skylight Studio.
Skylight Studio ni studio yenye vifaa vya kiwango cha kimataifa na imetengenezwa na Studio build International(UK) ambayo ni kampuni inayofanya kazi za ujenzi wa studio ya uingeleza.
Huu ni wimbo wa kwanza kufanyika ndani ya studio za Skylight Studio ambapo Skylight pia inatarajia kuzindua hivi karibuni kituo cha mafunzo kwa ajili ya vijana wenye vipaji vya muziki yaani Skylight Academy.
Kama ni mhudhuriaji wa matamasha ya Skylight hii ni ratiba yao kwenye msimu huu wa pasaka April 20 watakua Mwanza skylight beach resort(jembe beach) pia Tarehe  27 April watakua na tamasha Maalum la kutambulisha nyimbo mpya na wanamuziki wapya hili litafanyika pale Escape One.(Awadh Ibrahim)
Share:

Ijumaa, 4 Aprili 2014

MOVIE ZA LEO KATIKA UKUMBI WA SINEMAA

3_e593e.jpg
2_44cee.jpg
1_fd668.jpg
Movie ya Noah ambayo imekatazwa kuonyeshwa kwenye baadhi ya nchi, itaanza kuonekana kwenye theater za Tanzania kuanzia tarehe 4/4/2014.(AD)
Share:

MSANII KULALA NDANI YA TUMBO LA DUBU NI MAAJABU HAYA

DUBUUUU_c128c.jpg
Abraham Poincheval akichunguza ndani ya Dubu wake katika makavazi ya wanyama waliowindwa na kuhifadhiwa.
Msanii mmoja nchini Ufaransa anajiandaa kulala ndani ya tumbo la Dubu wake aliyewindwa na kuhifadhiwa katika makavazi ya wanyamapori mjini Paris.
Uamuzi wake huu umetajwa kama kuchagua kati ya maisha ya binadamu na wanyama.
DUBU2_1e666.jpg
Msanii huyo mfaransa anaanza maonyesho yake ya kiusanii ambayo yametajwa kuwa ya kipekee na ambayo yatashuhudia akilala ndani ya mnyama huyo kwa siku 13.
Abraham Poincheval aliyezaliwa mwaka 1972 kwa mara ya kwanza alifanya maonyesho hayo yanayojulikana kama -kuishi ndani ya ngozi ya Dubu- katika kituo cha maeonyeso ya usanii mjini Digne mwaka jana.
Sasa anajiandaa kurejelea onyesho hilo katika makavazi mjini Paris ambako atasalia ndani ya tumbo la Dubu huyo ambaye ni mnyama halisi isipokuwa tu amekaushwa na kuhifadhiwa katika makavazi hiyo.
Chanzo: BBC
(J M)
Share:

MGOGORO WASYRIA NI TISHIO KWA MASHARIKI YA KATI


iran_38c64.png
Afisa wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ametahadharisha kuwa kuendelea kwa muda mrefu mapigano ya wanamgambo wanaoungwa mkono na nchi za Magharibi nchini Syria ni hatari kwa usalama wa eneo zima la Mashariki ya Kati.
Hussein Amir-Abdollahian Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran anayeshughulikia masuala ya nchi za Kiarabu na Afrika amesema mgogoro unaoendelea nchini Syria ungeweza kutatuliwa iwapo silaha na wanamgambo wanaofadhiliwa na madola ya kigeni zingezuiwa kuingia nchini humo. (J.G)
Amir Abdollahian amesema hayo alipokutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Imarati Anwar Muhammad Qarqash na kuongeza kuwa, Jamhuri ya Kiislamu inaamini kuwa mazungumzo na majirani zake ndiyo njia inayofaa katika kupambana na ugaidi, makundi yenye kufurutu ada na migogoro ya kikaumu katika Mashariki ya Kati.
Kwa upande wake Qarqash amesema kuwa, mgogoro wa Syria hauwezi kutatuliwa kwa njia za kijeshi na kusisitiza kwamba suluhisho la kidiplomasia ndiyo njia pekee ya kutatua mgogoro huo
Share:

ZUIO LA BODABODA KATIKATI YA JIJI LA DAR ES LAAM LIANGALIWE UPYA


DSC 0054 7befc
Kumeibuka sintofahamu kubwa katika maeneo ya katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Hii ni kati ya wananchi wanaotumia usafiri wa pikipiki kwa ajili ya kuwahi maeneo yao ya kazi na askari wa kikosi cha usalama barabarani wanaosaidiana na maafisa wa kampuni moja binafsi iliyopewa jukumu la kuhakikisha kwamba amri ya kuzuia vyombo hivyo ingali ikitekelezwa.(Hudugu Ng'amilo)
Tayari kumeibuka malalamiko mengi kuhusiana na amri hiyo inayodaiwa kubarikiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, kwa kile kinachoelezwa kuwa ni njia mojawapo ya kupunguza vitendo vya uhalifu kama ujambazi katika maeneo ya katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Wapo wananchi wanaolalamikia uwapo wa faini zisizokuwa na ukomo, baadhi zikifikia hadi Sh. 50,000. Wapo wanaolia kwa kudai kukumbana na adha za kuombwa rushwa waziwazi. Kuna malalamiko vilevile yanayohusiana na ubabe uliokithiri
Wengine wanalalamika kuwa, utekelezaji wa zuio la bodaboda umekuwa chanzo cha usumbufu kwani waliopewa jukumu hilo hushindwa kutofautisha wenye bodaboda na raia wa kawaida wanaotumia pikipiki kwa matumizi yao binafsi na familia zao.
Kimsingi, sisi hatukubaliani na utaratibu unaotumika sasa. Tunadhani kwamba, hata kama kulikuwa na dhamira nzuri, lakini kinachoonekana ni kero dhidi ya wananchi.
Kwa mfano, NIPASHE tunaona kuwa uamuzi wa kuzuia bodaboda kwenye maeneo ya katikati ya jiji la Dar es Salaam haujatolewa katika kipindi sahihi.
Hii ni kutokana na ukweli kuwa hivi sasa, wakazi wa Dar es Salaam wako katika kipindi kigumu cha mpito, wakishuhudia miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara iliyosababisha maeneo mengi kutopitika kirahisi.
Kuna baadhi ya siku, safari fupi tu, kwa mfano kutoka Manzese hadi Posta, huwalazimu watumiaji wa barabara ya Morogoro kutumia hadi saa tatu ili kufika wanakokwenda. Adha ya foleni ni kubwa.
Ni dhahiri kuwa katika mazingira kama haya, usafiri wa pikipiki ndiyo suluhisho la pekee kwa wale wenye shughuli za dharura. Hivyo, Mamlaka za jiji kwa kushirikiana na vyombo vingine kama Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) na pia Jeshi la Polisi, vinapaswa kutambua kuwa huu si wakati mzuri wa kuzuia bodaboda kwenda katikati ya jiji na maeneo mengine pia.
Tunadhani vilevile kuwa, hata kama zuio hili likaendelea kubaki, basi ni vyema kukawa na utaratibu unaoeleweka wa kutofautisha waendesha bodaboda na watumiaji binafsi wa pikipiki.
Hali ya sasa si nzuri. Inawapa wananchi mateso na manyanyaso yasiyostahili kwa sababu wapo waliotozwa faini na kupotezewa muda wao mwingi barabarani kwa kudhaniwa kuwa ni watu wa bodaboda ilhali ukweli ni kwamba baadhi yao hubeba wake zao tu wakati wakiwahi kibaruani. Suala la usalama pia linahitaji ufafanuzi wa kina.
Hii ni kutokana na ukweli kuwa, kama bodaboda ni hatari kwa usalama katika maeneo ya Posta, basi hatari hiyo haiondoki pia katika maeneo mengine ya jiji kama Buguruni, Tegeta, Mwenge, Sinza, Kariakoo na Mbagala ambako pia kuna benki, maduka makubwa, ofisi za kampuni na shughuli nyingine za uzalishaji. Ni vyema amri hii ya kuzuia bodaboda katikati ya jiji ikatazmwa upya.
Tahadhari mvua kubwa,kimbunga visipuuzwe
KUNA tishio la kutokea mvua kubwa itakayoambatana na upepo mkali jijini Dar es Salaam na mikoa mingine ya Pwani ya Bahari ya Hindi ndani ya siku mbili zijazo.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya utabiri wa hali ya hewa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
NIPASHE tunashauri kuwa tahadhari hii isipuuzwe. Ifanyiwe kazi kuepuka maafa.
Kwa mfano, wakazi wa maeneo ya bondeni wanapaswa kuondoka mara moja.
Watumiaji wa vyombo vya majini wanapaswa kuwa makini pia katika siku hizi mbili ili kuepusha maafa ya kuzama kwa vyombo vyao kutokana na upepo mkali.
Shime, ile desturi ya kupuuza taarifa za wataalamu wa hali ya hewa iachwe mara moja. Ni hatari.
CHANZO: NIPASHE
Share:

WATAFANYA YAO NDAN YA DAR LIVE

Mafikizolo tayari washaingia ndani ya jiji la Dar es Salaam mchana huu. #MafikizoloLiveInDar
Photo: Mafikizolo tayari washaingia ndani ya jiji la Dar es Salaam mchana huu. #MafikizoloLiveInDar

Share:

HIKI NDIO KITAFANYIKA NEW MAISHA CLUB

Club-Maisha-4_8830e.jpg
New Maisha Club ndiyo Club pekee Tanzania iliyofanikiwa kuwa na matawi mengi mikoani ukitoa Dar es salaam ambayo ndiko ilikoanza,kwa sasa New Maisha Club ipo Morogoro,Mtwara,Dodoma na Mbeya ambapo kuna baaadhi ya party hufanyika siku moja kupitia club zote hizi.
IMG-20140403-WA00151_f3407.jpg
New Maisha Club 87.8 Mbeya Jumapili ya April 06 Kutakua na usiku wa vyuo ambao utasindikizwa na Roma Mkatoliki huko Roma ataenda pia kuzindua wimbo wake mpya wa K.K.K
shilole_074cb.jpg
New Maisha Club 88.5 Morogoro Jumapili April 06 kutakua na Shilole utakua ni uzinduzi wa video ya Chuna Buzi ambapo kwa Shilole atasindikizwa na Nuh Mziwanda na Darasa.
mirow_4eb77.jpg
New Maisha Club 88.4 Mtwara April 06 kutakuwa na Mirror kwenye Mirro’s Night upande wake atakua na Jordan da Prince.(AD)
Share:

Alhamisi, 3 Aprili 2014

MWALIMU AMUUA MWANAFUNZI


140403123409 mtoto akichapwa 304x171 bbc nocredit 6e3a5
Wazazi katika kaunti ya Kirinyaga mkoa wa Kati nchini Kenya wameandamana kwa hasira baada ya mwalimu kumchapa mtoto mmoja wa shule ya msingi hadi akafariki.(Hudugu Ng'amilo)

Mtoto huyo inaarifiwa alichapwa kichwani na mwalimu na kuzirai. Alifariki alipokuwa anapelekwa hospitalini.
Wazazi hao waliandamana kwa amani wakitaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya mwalimu huyo.
Hata hivyo polisi waliweza kumkamata mwalimu huyo na kumpeleka kituoni huku uchunguzi ukianza kufanywa.
Mtoto huyo alikuwa katika darasa la saba katika shule ya kibinafsi ya Roka Preparatory.
Inaarifiwa alizirai baada ya mwalimu kumchapa kwenye kisogo.
Wazazi hao waliokuwa wanalalamikia kile wanachosema ni wanafunzi kuadhibiwa vikali kwa makosa madogomadogo walitaka mwalimu huyo achukuliwe hatua kali kwa kitendo hicho cha kumchapa mwanafunzi ambacho kimeharamishwa katika shule zote nchini Kenya.
Wengi wa wazazi wenye watoto wao katika shule hiyo wameahidi kuwahamishia shule nyingine.
Kenya iliharamisha kitendo cha kuwachapa wanafunzi wa shule karibu miaka kumi iliyopita. Ilikuwa baada ya visa vya walimu kuwaadhibu vikali wanafunzi na kuwajeruhi kukithiri.
CHANZO BBC
Share:

MATUMIZI MABAYA YA POMBE


Na Martha Magessa
Asilimia 4 ya magongwa yasiyo ya maambukizi husababishwa na matumizi mabaya ya pombe kupita kiasi na kusababisha madhara mengi zaidi kwa watumiaji wa pombe ikiwemo mama mjamzito kuzaa mtoto kabla ya miezi tisa (Njiti)
Utafiti uliyofanyika oktoba 2012 ulibainisha kuwa asilimia 26.8 mpaka 31.9 sawa na watu milioni 15 Nchini Tanzania wanaotumia pombe na kati ya asilimia 27.4 ya wanaume wanywaji wa pombe ni walevi wa kupindukia na huku wanawake ikiwa ni asilimia 13.4.
Unywaji wa Pombe una hasara sana kuliko faida zake, hasara mbaya za pombe kwa mtumiaji ni upande wa kiafya.
Pombe ina hasara kwa binadamu kiuchumi na kusababisha umasikini kifamilia lakini kwa upande ndiyo zaidi hii inatokana kuwa mchango mkubwa katika kuleta magonjwa ingawa si kila ugonjwa husababisha na pombe pekee.
Madhara mengine ya unywaji wa pombe kupita kiasi husababisha ugonjwa wa Ini kwa kufa seli za Ini hivyo baadaye ini linapoteza uwezo kabisa, kwa hayo husababisha vifo vingi kwa ugonjwa huo.
Pombe husababisha kansa za tumbo na kansa ya Kongosho na mtumiaji wa pombe kwa kiasi kikubwa watoto huzaliwa katika hali ya utegemezi wa pombe kwa jina la kitaalam (Total alcoholic syndrome) ambayo hawezi kuweza kumpoteza mtoto ndani ya mwezi wa kwanza au kupata utahira wa kudumu katika tatizo la akili.
Vile vile pombe huathiri kiasi kikubwa kwa watumiaji mfumo wa uzazi na hata kupelekea mtumiaji kupoteza uwezo wa kuzaa kabisa na huanzia kwa kutopata siku za hedhi kwa mwanamke.
Madhara mengine ya utumiaji wa pombe kupita kiasi ni chanzo cha ajali za barabarani na kusababisha hasara kubwa kwa taifa kwa ujumla hali ambayo mpaka sasa watu milioni 2 Tanzania wamefariki dunia kwa sababu ya matumizi mabaya ya pombe.
Share:

Jumatano, 2 Aprili 2014

OBAMA AIONYA URUSI


Obama2_6a50e.jpg
Rais Obama yuko mjini Brussels ambapo atakutana na viongozi wa muungano wa Ulaya na shirika la kujihami la NATO, kuzungumzia mzozo wa Ukraine.
Kwenye hotuba muhimu kuhusu sera Rais Obama anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa usalama wa Marekani na nchi za Ulaya na pia kuonya Urusi dhidi ya kukiuka sheria za kimataifa.
Akizungumza mjini the Hague kabla ya kuelekea Brussel Rais Obama ameitaja hatua ya Urusi kutwaa eneo la Crimea kutoka kwa Ukraine kama ishara ya udhaifu.
Hatahivyo amesema bado kuna nafasi ya Urusi kusuluhisha mzozo huo kwa njia ya amani la sivyo ikabiliwe na vikwazo zaidi vya kiuchumi. Amesema japo huenda vikwazo hivyo vikaathiri uchumi wa dunia,Urusi ndio itakayoathirika zaidi.
Mkutano huo pia unatarajiwa kuzingatia maswala ya kibiashara na pia wasiwasi kwamba Marekani imekuwa ikichunguza kisiri shuguli za washirika wake kutoka nchi za Ulaya.(P.T)
Share:

Waziri asisitiza utunzaji wa vyanzo vya maji nchini


Profesa_Maghembe_Waziri_wa_Maji_51c73.png
Na Joel Mangoma
SERIKALI imesisitiza umuhimu wa utunzaji wa vyanzo vya maji kwa faida ya ustawi wa wananchi na maendeleo ya uchumi wa taifa kwa ujumla.
Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni mjini hapa na Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe, alipokuwa akiweka jiwe la msingi kwa ajili ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya Ziwa Victoria kutoka Kijiji cha Mhalo hadi mji wa Ngudu wilayani Kwimba.
Alisema lazima wananchi kutunza vyanzo vya maji ili kuepuka ukame unaoweza kutokea kutokana na uharibifu huo wa mazingira, na kwamba serikali inajitahidi kuhakikisha vyanzo vya maji vinalindwa ili kuepuka ukame.
"Tungependa wananchi wafahamu kuwa kutunza vyanzo vya maji ni kwa faida yao wenyewe, kwa vizazi vya sasa na vijavyo... kwa kufanya hivyo watajiwekea mazingira mazuri ya kujenga uchumi wa nchi.
"Rasilimali za maji zinapungua kwa kasi, hii yote ni kutokana na uharibifu wa mazingira," alisema Profesa Maghembe huku akitoa mifano ya maeneo kati ya mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Dodoma iliyokumbwa na uhaba wa maji.
Alisema wakati wa kiangazi maji yanakauka kwenye baadhi ya mito nchini jambo linaloleta hatari kwa afya ya binadamu na maisha ya viumbe majini na nchi kavu.
Akitoa mifano zaidi ya mito ambayo ilikuwa na maji na sasa imekauka, alisema maji yanayopita Dumila katika Mto Wami ni kidogo wakati kipindi cha nyuma maji yalikuwa yanapatikana kipindi chote cha mwaka bila kukauka.
"Ukipanda kwenye milima ya Usambara toka Korogwe hadi Bwiko utaona mito yote imekauka, mto pekee uliobaki ni ule wa Mkomazi, hii ni hatari," alisema waziri huyo.
Alielezea tatizo la mabadiliko ya tabia nchi husababisha upungufu wa maji katika maeneo mengi na kuwa maeneo yaliyokuwa yanapata milimita 1,000 kwa mwaka sasa hivi yanapata milimita 500.
Share:

Dk. Slaa avujisha siri

slaa_37b27.jpg
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, amesema wamenasa nyaraka na viashiria mbalimbali vinavyoonyesha kuwa Chama Cha Mapinduzi kinakusudia kuharibu mchakato wa katiba.
Dk. Slaa, alitoa kauli hiyo juzi usiku jijini Mwanza katika kipindi cha ‘Ajenda 2015’, kinachorushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Star Tv.
Kiongozi huyo alikuwa akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hicho, Dotto Bulendu, aliyetaka kujua ni kwanini Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) wameamua kuanza ziara mikoani kuwaelimisha wananchi wakati mchakato wa katiba ndio upo katika hatua ya rasimu ya pili kujadiliwa bungeni.
Akijibu swali hilo, Dk. Slaa, alisema wananchi wamechanganywa kwa kuwa waliambiwa wakusanye maoni yao na kuyapeleka katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyokuwa chini ya Jaji Joseph Warioba, lakini Rais Jakaya Kikwete kaidharau.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete alipoenda kuzindua Bunge, alitumia muda huo kutoa semina elekezi na kutangaza msimamo wa Chama Cha Mapinduzi ambao haukujali maoni ya wananchi,” alisema Dk. Slaa.
Alisema Watanzania wanapaswa kuelewa kuwa CHADEMA walipokuwa wanapigania sheria ya mabadiliko ya katiba kutaka rais asiwe na mamlaka makubwa katika kuteua wajumbe wa Bunge Maalumu, walibaini athari za mchakato kutekwa na chama tawala.
Alibainisha kuwa msemaji wa kambi rasmi ya upinzani kuhusu mambo ya katiba na sheria, Tundu Lissu, aliyekuwa akipinga jambo hilo, alionekana ni mbishi, asiyependa kuwasikiliza wengine, lakini athari ya uteuzi inaonekana sasa.
Dk. Slaa, alisema wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba asilimia kubwa ni wanachama wa CCM kwa kivuli cha kupitia kwenye asasi mbalimbali.
Alisema vyama vinavyounda Ukawa, vimeamua kwenda kwa wananchi nchi nzima kuwaeleza ukiukwaji wa kanuni uliofanywa kwa makusudi na Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta, ambaye aliruhusu Jaji Warioba awasilishe rasimu kabla ya hotuba ya ufunguzi ya Rais Kikwete.
Alibainisha kuwa kilichofanywa na Sitta kililenga kutoa fursa kwa Rais Kikwete kuwachanganya wananchi kwa kupinga maoni ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba aliyoiunda.
Dk. Slaa, aliongeza kuwa Ukawa wamejitokeza sasa kutokana na serikali kutumia nguvu nyingi ikiwemo vyombo vya habari kuchakachua maoni ya wananchi.
“Tume ni ya rais mwenyewe, ilitumwa kukusanya maoni na yeye mwenyewe, hadidu za rejea alitoa yeye, na ushahidi upo amefanya mahojiano ya mara kwa mara na tume, hivyo kuja kukataa maoni ya wananchi, ni dharau na matusi kwa Watanzania waliotoa maoni,” aliongeza Dk. Slaa.
Dk. Slaa, alikemea matamko yanayotolewa na baadhi ya watu kukataa kuheshimu maoni ya wananchi, akitolea mfano kauli ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana aliyoitoa wiki iliyopita katika viwanja vya Mwembeyanga, Temeke jijini Dar es Salaam.
Akihutubia mkutano wa wanachama wa CCM, Kinana alikaririwa akisema; “mchakato wa katiba mpya unaoendelea bungeni mjini Dodoma,   msimamo wa CCM utaendelea kuwa ni serikali mbili.”
Alisema hotuba iliyotolewa na Rais Kikwete, wakati akizindua Bunge la Katiba, imetoa mwelekeo mpya kwa wajumbe wa Bunge.
Mchangiaji mwingine katika kipindi hicho aliyejulikana kama Solomon Lufunda aliyekuwa katika kipindi hicho upande wa Dar es Salaam, alisema kuwa mchakato wa katiba umeingiliwa zaidi na serikali na kuwanyima wananchi fursa.
Lufunda alisema kuwa CCM imeingilia na inavuruga mchakato wa katiba, haiheshimu matakwa ya wananachi.
Alikemea vikali kauli ya hofu iliyosemwa na Rais Kikwete kuwa endapo wananchi wataunga mkono serikali tatu, basi jeshi litapindua serikali na kuongoza nchi, au kuleta machafuko nchini.
Mara baada ya uteuzi wa wajumbe wa Bunge la Maalumu la Katiba, Mbunge wa Singida Mashariki ambaye ndiye msemaji katika suala la katiba na sheria, Lissu, alinukuliwa akisema:
“Sisi CHADEMA tulisema tangu mwanzo kuwa tukimuachia Rais Jakaya Kikwete afanye uteuzi ni kuhalalisha kupata katiba ya ubabaishaji, na hili linaashiria kutokea baada ya wajumbe wa CCM kuwa wengi kuliko vyama vingine.”
Alisema wajumbe walioteuliwa wanaonyesha namna gani wanavyorudisha asante kwa Rais Kikwete kutokana na kuteuliwa katika nafasi hiyo, dalili inayoonyesha kuwa wajumbe hao  ni watu wake na wataenda kutekeleza masilahi yake badala ya wananchi.
Lissu alisema licha ya wajumbe wengi kuonyesha wazi kuwa na masilahi na Rais Kikwete, CHADEMA itapambana kuhakikisha kuwa katiba inayopatikana inakuwa kwa masilahi ya wananchi na si wanasiasa.
(J.G)
Share:

MATUKIO YA VIDEO

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text