Kumeibuka sintofahamu kubwa katika maeneo ya katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Hii ni
kati ya wananchi wanaotumia usafiri wa pikipiki kwa ajili ya kuwahi
maeneo yao ya kazi na askari wa kikosi cha usalama barabarani
wanaosaidiana na maafisa wa kampuni moja binafsi iliyopewa jukumu la
kuhakikisha kwamba amri ya kuzuia vyombo hivyo ingali ikitekelezwa.(Hudugu Ng'amilo)
Tayari
kumeibuka malalamiko mengi kuhusiana na amri hiyo inayodaiwa kubarikiwa
na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa, kwa kile kinachoelezwa kuwa ni
njia mojawapo ya kupunguza vitendo vya uhalifu kama ujambazi katika
maeneo ya katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Wapo
wananchi wanaolalamikia uwapo wa faini zisizokuwa na ukomo, baadhi
zikifikia hadi Sh. 50,000. Wapo wanaolia kwa kudai kukumbana na adha za
kuombwa rushwa waziwazi. Kuna malalamiko vilevile yanayohusiana na ubabe
uliokithiri
Wengine
wanalalamika kuwa, utekelezaji wa zuio la bodaboda umekuwa chanzo cha
usumbufu kwani waliopewa jukumu hilo hushindwa kutofautisha wenye
bodaboda na raia wa kawaida wanaotumia pikipiki kwa matumizi yao binafsi
na familia zao.
Kimsingi,
sisi hatukubaliani na utaratibu unaotumika sasa. Tunadhani kwamba, hata
kama kulikuwa na dhamira nzuri, lakini kinachoonekana ni kero dhidi ya
wananchi.
Kwa
mfano, NIPASHE tunaona kuwa uamuzi wa kuzuia bodaboda kwenye maeneo ya
katikati ya jiji la Dar es Salaam haujatolewa katika kipindi sahihi.
Hii ni
kutokana na ukweli kuwa hivi sasa, wakazi wa Dar es Salaam wako katika
kipindi kigumu cha mpito, wakishuhudia miradi mikubwa ya ujenzi wa
barabara iliyosababisha maeneo mengi kutopitika kirahisi.
Kuna baadhi ya siku, safari fupi tu, kwa mfano kutoka Manzese hadi Posta, huwalazimu watumiaji wa barabara ya Morogoro kutumia hadi saa tatu ili kufika wanakokwenda. Adha ya foleni ni kubwa.
Kuna baadhi ya siku, safari fupi tu, kwa mfano kutoka Manzese hadi Posta, huwalazimu watumiaji wa barabara ya Morogoro kutumia hadi saa tatu ili kufika wanakokwenda. Adha ya foleni ni kubwa.
Ni
dhahiri kuwa katika mazingira kama haya, usafiri wa pikipiki ndiyo
suluhisho la pekee kwa wale wenye shughuli za dharura. Hivyo, Mamlaka za
jiji kwa kushirikiana na vyombo vingine kama Mamlaka ya Udhibiti wa
Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) na pia Jeshi la Polisi,
vinapaswa kutambua kuwa huu si wakati mzuri wa kuzuia bodaboda kwenda
katikati ya jiji na maeneo mengine pia.
Tunadhani
vilevile kuwa, hata kama zuio hili likaendelea kubaki, basi ni vyema
kukawa na utaratibu unaoeleweka wa kutofautisha waendesha bodaboda na
watumiaji binafsi wa pikipiki.
Hali ya
sasa si nzuri. Inawapa wananchi mateso na manyanyaso yasiyostahili kwa
sababu wapo waliotozwa faini na kupotezewa muda wao mwingi barabarani
kwa kudhaniwa kuwa ni watu wa bodaboda ilhali ukweli ni kwamba baadhi
yao hubeba wake zao tu wakati wakiwahi kibaruani. Suala la usalama pia
linahitaji ufafanuzi wa kina.
Hii ni
kutokana na ukweli kuwa, kama bodaboda ni hatari kwa usalama katika
maeneo ya Posta, basi hatari hiyo haiondoki pia katika maeneo mengine ya
jiji kama Buguruni, Tegeta, Mwenge, Sinza, Kariakoo na Mbagala ambako
pia kuna benki, maduka makubwa, ofisi za kampuni na shughuli nyingine za
uzalishaji. Ni vyema amri hii ya kuzuia bodaboda katikati ya jiji
ikatazmwa upya.
Tahadhari mvua kubwa,kimbunga visipuuzwe
KUNA tishio la kutokea mvua kubwa itakayoambatana na upepo mkali jijini Dar es Salaam na mikoa mingine ya Pwani ya Bahari ya Hindi ndani ya siku mbili zijazo.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya utabiri wa hali ya hewa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
KUNA tishio la kutokea mvua kubwa itakayoambatana na upepo mkali jijini Dar es Salaam na mikoa mingine ya Pwani ya Bahari ya Hindi ndani ya siku mbili zijazo.
Hii ni kwa mujibu wa taarifa ya utabiri wa hali ya hewa iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
NIPASHE tunashauri kuwa tahadhari hii isipuuzwe. Ifanyiwe kazi kuepuka maafa.
Kwa mfano, wakazi wa maeneo ya bondeni wanapaswa kuondoka mara moja.
Watumiaji
wa vyombo vya majini wanapaswa kuwa makini pia katika siku hizi mbili
ili kuepusha maafa ya kuzama kwa vyombo vyao kutokana na upepo mkali.
Shime, ile desturi ya kupuuza taarifa za wataalamu wa hali ya hewa iachwe mara moja. Ni hatari.
Shime, ile desturi ya kupuuza taarifa za wataalamu wa hali ya hewa iachwe mara moja. Ni hatari.
CHANZO: NIPASHE
0 maoni:
Chapisha Maoni