Jumatano, 16 Aprili 2014

KIMEWAKA HUKO MJINI DODOMA BUNGENI



SHEKHE wa Mkoa wa Dodoma Mustapha Rajabu amewataka wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wanaowakilisha kupitia taasisi zao kwenye mchakato wa kuipata Katiba mpya kutokubali kununuliwa na wawakilishi wa vyama vya siasa.
Alisema hayo hivi karibuni wakati akizungumza kwenye chakula cha pamoja kati ya watoto yatima na wajane kilichoandaliwa na Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) kata ya Chang’ombe mjini hapa.
Alisema wajumbe hao wanaotoka uwakilishi wa taasisi mbalimbali ndani ya Bunge hilo wanatakiwa kutoa mawazo ambayo yatanufaisha na kuwagusa Watanzania wote na siyo yenye mtazamo wa itikadi za kichama kama wanavyotaka wanasiasa hao.
Kiongozi huyo wa dini alisema wawakilishi hao wamechaguliwa kwa ajili ya kupendekeza mahitaji yao kwenye katiba hiyo, hivyo wasikubali kununuliwa na vyama vya siasa ambavyo vinataka kuingiza itikadi za kisiasa ndani ya katiba.(Martha Magessa)
Pia amelitaka Bunge hilo kutopoteza muda kwa ajili ya malumbano yasiyokuwa na hoja muhimu ambayo yamekuwa yakiwakera watanzania ambao wanaisubiri Katiba itakayoboresha maisha ya wananchi.
Alisema inasikitisha kuona na kusikia kupitia vyombo vya habari wabunge hao wakichukua muda mwingi, kukashifiana na kulumbana kwani huko ni kupoteza muda huku wajumbe hao wakiendelea kupata posho bila kufikia maamuzi yatakayotengeneza hiyo Katiba.
Awali akisoma risala kwa niaba ya watoto yatima na wajane Mwenyekiti wa Baraza hilo, kata ya Chang’ombe Salumu Mabada, aliwataka wajumbe maalumu wa Bunge la Katiba kuendelea kuhubiri amani na upendo kwa muda wote wanapokuwa ndani na nje ya kikao badala ya kupandikiza chuki na migogoro na hatimaye kuleta mafarakano kwenye mchakato mzima unaoendelea wa kuipata katiba.
Aidha aliwataka wajumbe hao ambao miongoni mwao wanatoka taasisi za kidini, kuendelea kumtanguliza Mungu ili amani itawale na hatima Katiba ipatikane yenye kukubalika na watu wote. 
CHANZO:HABARILEO
Share:

0 maoni:

MATUKIO YA VIDEO

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text