
Rais
Obama yuko mjini Brussels ambapo atakutana na viongozi wa muungano wa
Ulaya na shirika la kujihami la NATO, kuzungumzia mzozo wa Ukraine.
Kwenye
hotuba muhimu kuhusu sera Rais Obama anatarajiwa kusisitiza umuhimu wa
usalama wa Marekani na nchi za Ulaya na pia kuonya Urusi dhidi ya
kukiuka sheria za kimataifa.
Akizungumza
mjini the Hague kabla ya kuelekea Brussel Rais Obama ameitaja hatua ya
Urusi kutwaa eneo la Crimea kutoka kwa Ukraine kama ishara ya udhaifu.
Hatahivyo
amesema bado kuna nafasi ya Urusi kusuluhisha mzozo huo kwa njia ya
amani la sivyo ikabiliwe na vikwazo zaidi vya kiuchumi. Amesema japo
huenda vikwazo hivyo vikaathiri uchumi wa dunia,Urusi ndio
itakayoathirika zaidi.
Mkutano
huo pia unatarajiwa kuzingatia maswala ya kibiashara na pia wasiwasi
kwamba Marekani imekuwa ikichunguza kisiri shuguli za washirika wake
kutoka nchi za Ulaya.(P.T)
0 maoni:
Chapisha Maoni