Jumanne, 30 Desemba 2014

MAMA APATA UCHUNGU NDANI YA TRENI MAPOLISI WAWAJIBIKA KUVAA JUKUMU LA UKUNGA...PATA STORY KAMILI...

5502080-Shenyang_Train_Station-0Katika siku ya christmas watoto wengi walizaliwa katika siku hiyo, lakini mtoto huyu alizaliwa mazingira ambayo wengi walionekana kushangazwa.
Maafisa wawili wa Polisi Daniel Caban na Darrell James walipewa taarifa ya kutakiwa kutoa msaada wa dharura katika treni ya abiria Philadelphia, walipofika waligundua kwamba dharura yenyewe ni mwanamke ambaye alikuwa katika hali ya kukariba kujifungua, muda haukuruhusu kumkimbiza Hospitali.
Walimsaidia mwanamke huyo kujifungua salama mtoto wa kiume na baadaye wakapelekwa Hospitali ya Hahnemann University wote wakiwa na hali nzuri.
Afisa mmoja amesema alikuwa ameshafungua zawadi zake zote kwa ajili ya siku hiyo na hakujua kama kuna zawadi nyingine ambayo ilikuwa inamsubiria aifungue.
Tukio kama hili liliwahi kutokea mwaka jana baada ya mwanamke mmoja kujifungua mtoto wa kike akiwa kwenye treni ya abiria London lakini yeye alipata bahati ya kusaidiwa na mkunga ambaye alikuwa ndani ya treni hiyo pia.
cegrab-20141226-121733-139-1-480x360

Share:

0 maoni:

MATUKIO YA VIDEO

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text