
Imezungumzia sana kuwa Kim Kardashian na Kanye West wanakosa muda wa kukaa pamoja kutokana na ‘Ubusy’ alionao Kanye hali inayosababisha mara nyingi kushinda studio akirekodi kazi zake.
Sasa malalamiko hayo kwa mkewe yanaweza kuwa yamefikia kikomo baada ya wawili hawa kuamu kununua jumba lingine la kifahari la jirani yao katika jiji la Los Angeleslenye thamani ya dola za Marekani milioni 3 kwa lengo la kuongeza mali zao zenye utajiri wa zaidi ya dola za Marekani milioni 20.

Wawili hao wamepanga kufanyia matengenezo katika nyumba hiyo ambapo kutakua na sehemu kwa ajili ya watoto wao,uwanja wa basketball,sehemu ya kuangalia filamu,sehemu ya michezo,spa kwa ajili ya Kim,eneo la wageni pamoja na studio itakayokua maalum kwa ajili ya Kanye kumsaidia kutokwenda sehemu nyingine yoyote kurekodi kazi zake.
0 maoni:
Chapisha Maoni