Siku
moja baada ya kuachiwa huru kwa yule mwanamke aliyekuwa amehukumiwa
kifo kwa kosa la kuolewa na mwanaume wa kikristo,Taarifa kutoka nchini
Sudan zinasema kuwa mwanamke huyo amekamatwa tena.
Jina
lake ni Meriam Ibrahim,alikamatwa akiwa na familia yake katika uwanja
wa ndege mjini Khartoum,watu waliomkamata walikuwa wamevalia mavazi ya
kiraia ingawa wanaaminika kuwa ni wanajeshi wa Serikali.Duru zinasema kuwa Meriam Ibrahim aliyejifungulia jela alikuwa anajiandaa kuondoka nchini Sudan pamoja na familia yake mpaka sasa haijajulikana kwa nini alikamatwa na karibu watu arobaini waliokuwa wamavalia mavazi ya kiraia siku moja tu baada ya kuachiliwa kuambatana na uamuzi wa mahakama ya rufaa.
Meriam alikamatwa mara ya kwanza mwezi Februari na kujifungulia mtoto wake wakike akiwa jela baada ya kuhukumiwa.






0 maoni:
Chapisha Maoni