Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Na Mwandishi wetu – Hazina
Dhana
ya kukua katika maisha ya jamii inahusisha mtu, Wizara, Idara naTaasisi
mbalimbali zinazounda jumuiya ya watu au taifa fulani.
Ni
ukweli usiopingika kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekua na
kufikisha umri wa nusu karne ambapo Aprili 26 mwaka huu wa 2014
inajivunia kufikisha miaka 50 tangu kuasisiwa kwake (1964- 2014).
Sherehe
za Maadhimisho ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ziliongozwa na
kupambwa na kauli mbiu inayosema “Utanzania wetu ni Muungano wetu,
tuulinde, tuuimarishe na kuudumisha”.
Tunapoadhimisha
sherehe ya dhahabu ya muungano huu, Wizara ya Fedha inajivunia
mafanikio makubwa ikiwa nimoja kati ya Wizara muhimu katika muungano
huo.
Serikali
ya Awamu ya Nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na
Jemedari wake Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ndio msimamizi mkuu wa
Wizara, Idara na taasisi zinazoshughulikia muungano huu adhimu Afrika na
dunia nzima.
Dhana
ya kukua Wizara ya Fedha imejitokeza tangu kuundwa kwa Muungano mwaka
1964, ambapo Wizara hiyo imekuwa na majina tofauti kulingana na majukumu
inayopewa kwa wakati husika.
Majina
hayo ni Wizara ya Fedha (1962 – 1966), Wizara ya Fedha na Mipango
(1977), Wizara ya Nchi, Mipango na Uchumi (1983), Wizara ya Fedha na
Uchumi (2008) na Wizara ya Fedha (2010).
Mabadiliko
ya majina haya yalienda sanjari na mabadiliko ya muundo na majukumu ya
Wizara ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa Idara na vitengo mbalimbali
kwa lengo la kuchangia uboreshaji wa ufanisi katika uendeshaji wa
shughuli za Serikali.
Idara
na taasisi hizo ni pamoja na Idara ya Uchambuzi wa Sera – Kitengo cha
Sera za Madeni, Kitengo cha Kudhibiti Fedha Haramu (FIU), Benki Kuu ya
Tanzania, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Ofisi ya Taifa ya Takwimu
(NBS) na Tume ya Pamoja ya Fedha.
Wizara
hii katika kutekeleza majukumu yake imekuwa na mafanikio mengi kupitia
Taasisi, Idara na Vitengo mbalimbali vilivyo chini yake.
Miongoni mwa mafanikio hayo yanatokana na juhudi na maarifa ya kutekeleza majukumu kupitia Taasisi, Idara na Vitengo vyake.
Idara
ya Uchambuzi wa Sera – Kitengo cha Sera za Madeni katika kipindi cha
miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Idara ya Fedha za Nje
imeweza kutekeleza kwa mafanikio majukumu yaliyo chini ya idara hizo.
Kwa
kipindi chote cha miaka 50 uchambuzi wa deni la Taifa uliofanyika mwezi
Septemba, 2013 unaonesha kwamba deni la Taifa limeendelea kuwa
himilivu.
Uhimilivu
huo wadeni la Taifa unaonekana kupitia viashiria mbalimbali
vilivyowekwa na kukubaliwa kimataifa. Vinavyohusisha deni la Taifa na
Pato la Taifa , mapato ya ndani na mauzo ya nje ya nchi.
Matokeo
ya uchambuzi wa uhimilivu wa deni la taifa kama inavyoonekana kwa
uwiano wa thamani ya sasa ya deni la Nje kwa Pato la Taifa kwa mwaka
2013 unaonesha ulikuwa ni asilimia 24.8 wakati na ukomo wake ni
asilimia 50.
Uwiano
wa thamani ya sasa ya deni la nje kwa thamani ya mauzo nje ya Nchi ni
asilimia 98.3 na ukomo wake ni asilimia 200. Uwiano wa Thamani ya sasa
ya deni la nje kwa Mapato ya Ndani ni asilimia 121.2 na ukomo wake ni
asilimia 300.
Pia
Uwiano wa Ulipaji wa deni la nje ikilinganishwa na thamani ya Mauzo ya
bidhaa Nje ya Nchi asilimia 3.3 na ukomo wake ni asilimia 25.
Uwiano
wa Ulipaji wa Deni ikilinganishwa na Mapato ya ndani ni asilimia 4.3 na
ukomo wake ni asilimia 22 wakati Thamani ya sasa ya deni la Serikali
ikilinganishwa na Uwiano wa Pato la Taifa ni asilimia 40.5 na ukomo
wake ni asilimia 74.
Tangu
kuasisiwa kwa muungano, Tanzania imeendelea kuwa na mafanikio makubwa
katika matumizi ya misaada na mikopo kutoka Ndani na Nje ya nchi katika
kujiletea maendeleo yake.
Katika
kipindi chote cha Muungano, Wizara ya Fedha imeendelea kutekeleza
miradi mbalimbali kwa kutumia misaada na mikopo inayopokelewa kutoka kwa
wahisani na taasisi za fedha kutoka Ndani na Nje ya nchi.
Baadhi
ya miradi iliyotekelezwa kupitia misaada na mikopo hiyo katika matumizi
mbalimbali kwa pande mbili za Muunganoni pamoja na usambazaji wa maji
kutoka Ruvu Chini kwenda Miji ya Chalinze, Pwani, Dar es salaam, Unguja
na Pemba.
Kwa
upande wa elimu, Wizara ya Fedha imesimamia utekelezaji wa ujenzi wa
vyuo vikuu nchini miongoni mwao ikiwa ni Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA).
Miradi mingine ya Elimu ni ujenzi wa shule za sekondari za Kimuteni Unguja na Mkanyageni Pemba.
Kwa
upande waMawasiliano, Wizara kupitia wahisani ilipokea misaada
mbalimbali, na kufanikiwa kuboresha miradi ya Tehama ambapoMkongo wa
Taifa umejengwa Tanzania Barana kuwezesha kuwepo kwaSerikali mtandao
Zanzibar.
Katika
kuhakikisha askari wanapata na kuwajengea mazingira mazuri ya kazi,
Wizara imefanikiwa kusimamia utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za makazi
ya askari polisi maeneo ya barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaa pamoja
naUnguja na Pemba.
Miradi mingine iliyotekelezwa kupitia Wizara ya Fedha niujenzi na ukarabati wa barabara mbalimbali nchini.
Barabara
hizo ni pamoja na zilizoko Pemba ambazo ni barabara za Wete – Gando,
Wete – Konde, Raha – Hukunjwi, Mtuhaliwa – Chake na kwa upande wa Unguja
barabara za Kidmni – Kitope na Machui – Ring.
Kwa
upande wa Tanzania Bara, barabara zilizojengwa na kukarabatiwa kupitia
Wizara ya Fedha ni pamoja na barabara ya Dar es Salaam hadi Dodoma,
Chalinze hadi Segera na Dar es Salaam kupitia Lindi hadi Mtwara.
Kwa
kuwa kilimoni uti wa mgongo wa taifa, Wizara ya Fedha imekuwa ikipokea
misaada na mikopo mbalimbali na kuielekeza kwenye Wizara husika ili
iweze kusimamia miradi iliyokusudiwa.
Miradi
ya Kuendeleza Kilimohaikuachwa nyuma ambapokilimocha mpunga kwa njia ya
umwagiliaji kinatekelezwa Zanzibar, Kilimanjaro, Morogoro.Kumekuwepo
pia na usambazaji wa mbolea kwa wakulima katika pande zote mbili za
muungano ili kuboresha uzalishaji na kuongeza tija kwa mazao ya chakula
na biashara na hivyo kuleta maendeleo endelevu ya taifa kwa lengo la
kuiwezesha nchi ifikie uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
Mafanikio
haya ya Wizara yanatokana na msingi imara uliojengeka ndani ya
watumishi kwa kuzingatia taaluma zao, ubunifu, kuwajali wageni na wateja
wanaofika ofisini kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali ofisini humo,
kujitoa kufanya kazi kwa moyo kwa kuzingatia weledi wa taaluma zao na
kwa kufuata maadili ya utumishi wa umma na kutoa huduma hizo kwa wakati.
Mafanikio
haya yanatokana nausimamizi mzuri wa sera za uchumi ili kuweka
mazingira mazuri ya kisera kwa lengo la kuwezesha kufikiwa kwa malengo
ya maendeleo ya Taifa.
Ili
Wizara iendelee kufanya vizuri katika kumhudumia Mtanzania, inaendelea
kuandaa mafunzo mbalimbali ya muda mfupi na mrefu kwa mujibu wa
mahitaji.
Kwa
kuzingatia umuhimu wa rasilimali watu, Wizara imejipanga kufanikisha
uendelezaji wa watumishi kwa kuwaongezea ujuzi na maarifa ya ukusanyaji,
uchambuzi na uwasilishaji wa takwimu zinazoonesha hali halisi ya
maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini.
Tukubali
kuwa “Palipo na nia pana njia”, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
inaheshimu na kuzingatia misingi ya utu, uhuru, haki, usawa, udugu,
amani, umoja, na mshikamano katika nyanja zote za maisha yetu.
Hali
hii itaifanya nchi isonge mbele na Muungano uendelee kuimarika na
kuufanya kuwa ni mfano wa kuigwa kwa mataifa mengine Afrika na Dunia kwa
ujumla, ndio maana wimbo wetu wa taifa unadhihirisha nchi yetu
kudumisha uhuru na umoja.
Hivyo
Tanzania ni moja, na watu wake ni wamoja ni wajibu wetu sote kuimarisha
na kudumisha uzalendo wa Taifa miongoni mwa Watanzania ili kuendeleza
dhamira yetu ya kulinda, kuimarisha na kudumisha Muungano ulioasisiwa
kwa kuchanganya udongo wa Tanganyika na Zanzibar.
0 maoni:
Chapisha Maoni