
Msanii Mb Dog pichani.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
MWIMBAJI
wa muziki wa kizazi kipya, Mbwana Mohamed Mb Dog, amekamilisha nyimbo
nyingine mbili mpya zinazojulikana kama “Ya Moto” na “Demu Mwingine”.
Kukamilika
kwa nyimbo hizo ni mwendelezo wa mikakati ya msanii huyo kufanya kazi
nzuri ili kumuweka katika kiwango cha juu katika tasnia ya muziki wa
kizazi kipya.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam, Mb Dog alisema kwamba nyimbo hizo amezirekodi
katika Studio yake ya Macoppa, zilizopo jijini Dar es Salaam.
Alisema
kuwa nyimbo hizo zinaungana na ile ‘Mbona Umenuna’ aliyoachia mapema
mwezi uliopita na kupokewa kwa shangwe na wadau wa Bongo Fleva Tanzania.
“Hizi ni nyimbo mbili mpya na ambazo naamini zitapokewa kwa shangwe na wadau mbalimbali wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini.
“Naamini
kila kitu kitakwenda vizuri kuhakikisha kuwa mambo yanakuwa mazuri,
ukizingatia kuwa mipango iliyopo mbele yangu ni kufanya kazi ya maana
ili nionyeshe ukomavu wangu kisanaa,” alisema Mb Dog.
Mb
Dog ni mmoja wa wasanii wanaotambulika kwa umahiri wao katika tasnia ya
Bongo Fleva, huku akikumbukwa kwa nyimbo zake, ukiwamo ule wa Latifa na
nyinginezo
0 maoni:
Chapisha Maoni