Jumamosi, 15 Novemba 2014

HAYA MAKUBWA HAYA .....HIVI NDIVYO VOCHA ILIVYOWEZA KUHATARISHA MAISHA YA MTU....PATA STORY KAMILI.

phone
Mwanamke mmoja amenusurika kuuwawa kutokana na kupigwa na mume wake ambaye ni askari, kisa ikiwa ni mwanamke huyo kushindwa kumnunulia vocha.
Akisimulia mkasa huo mke wa askari huyo Eva Okoth, amesema mume wake alikuwa ametoka kunywa pombe na rafiki zake, akaanza kujisikia vibaya baada ya kushindwa kula na kutapika akihisi rafiki zake walimwekea sumu katika pombe, hivyo akampatia hela mke wake ili akanunue vocha kuwapigia ndugu zake ili awaage kwamba anakufa.
Mwanamke huyo anasema wakati huo ilikuwa saa 11 alfajiri, maduka yalikuwa hayajafunguliwa, askari huyo alichukua bunduki na kuanza kufyatua risasi huku akitishia kumuua na kujiua yeye.
Eva alikimbia kujificha jikoni, taarifa kutoka kwa msemaji wa kituo cha Polisi Lameck Kigozi amemtambua askari huyo kuwa ni John Okoth na kueleza kuwa baada ya askari wenzake kusikia milio ya risasi walikimbilia katika nyumba ya askari huyo na alipowaona aliendelea kuwarushia risasi japo hakuna aliyedhurika.
Share:

0 maoni:

MATUKIO YA VIDEO

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text