
Waandishi wa Habari hao Peter Greste raia wa Australia, Mohammed Fahmy mwenye asili ya Canada na Baher Mohammed wanashikiliwa Misri ambako walihukumiwa kifungo baada ya kukutwa na hatia ya kukisaidia chama cha Muslim Brotherhood na kueneza habari za kupendelea upande wa Kikundi hicho.
Rais wa Misri, Abdi Fatah El Sisi amesema msamaha huo utatolewa kama hakutakuwa na athari yoyote kwa nchi hiyo kiusalama.
Waandishi wawili kati yao walihukumiwa kifungo cha miaka 10, mmoja wao akihukumiwa kifungo cha miaka 7
0 maoni:
Chapisha Maoni