Alhamisi, 30 Oktoba 2014

UCHUNGU WA WAZAZI HAWA KWA WATOTO WAO UMEFIKIA KIWANGO HIKI......

Wazazi Kulinda ShuleKuna ukweli kwenye msemo wa waswahili unaosema “uchungu wa mwana aujuaye mzazi”, na ndio maana stori nnayokuletea huenda ikawa ngeni na hujawahi kukutana nayo, lakini wazazi hawa wameonesha namna walivyo na uchungu kwa vitendo na sio maneno pekee.
Stori kutoka Kenya inahusu kitendo cha wazazi kuamua kujichukulia jukumu la ulinzi wa eneo la shule ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu ambavyo vimekuwa vinajitokeza mara kwa mara katika maeneo hayo.
Kila jioni Esuruan Awet ni moja ya wazazi hao ambao hujiunga na kikundi cha askari Polisi wa akiba kwa lengo la kupiga doria eneo la shule ya msingi Nakatong’wa, Mashariki mwa Turkana huko Kenya.
Eneo la shule hiyo limekuwa likikabiliwa na matukio ya kuvamiwa mara kwa mara kitendo kilichowafanya wazazi hao kujiunga na kikosi hicho kukabiliana na uhalifu huo.
Share:

0 maoni:

MATUKIO YA VIDEO

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text