Alhamisi, 21 Agosti 2014

KUHUSU WATU 16 WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA GARI HUKO MKOANI TABORA



Watu16 wamekufa papo hapo baada ya mabasi mawili kugongana uso kwa uso huko katika kijiji cha murogoro wilayani sikonge mkoani Tabora katika kile kilichodaiwa kuwa ni kutochukua tahadhari Madereva wakati wa kupishana kwenye barabara za vumbi.
Kamanda wa polisi mkoani tabora kamishina msaidizi Suzani kaganda amesema kuwa, ajali hiyo iliyotokea jana jioni, imehusisha mabasi ya sabena lenye namba za usajili T 110 AVR scania, lililokuwa likitoka jijini Mbeya kuelekea mkoni Tabora, na basi la kampuni ya AM Coach lenye namba za usajili T 803 AGN lililokuwa likitokea jijini mwanza kuelekea wilayani mpanda mkoani katavi.
Aidha amesema kuwa, mabasi hayo yaligongana uso kwa uso kutokana na vumbi kubwa lililokuwa limetokea baada ya kupishana na gari jingine, marehemu hao waliotambulika ni 10 wakiwemo Madereva wa magari hayo, Aristides Shirima, aliyekuwa akiendesha basi la AM,, na James Komba aliyekuwa akiendesha basi la Sabena, ambapo amesema kuwa, wananchi wanaweza kufika katika hospitali ya Sikonge kwa utambuzi wa marehemu.
Waliofariki katika ajali hiyo ni wanaume 10, wanawake wanne na watoto wawili ambapo mmoja akiwa na umri unaodhaniwa kuwa miezi saba na nane, na mwingine miaka 8-10
Share:

0 maoni:

MATUKIO YA VIDEO

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text