Shindano la Big brother Africa mwaka 2013 ndio liliifanya Afrika ikamfahamu mtu anaitwa Feza Kessy ambae siku kadhaa kabla ya kujiunga na washiriki wenzake kwenye hilo jumba alikua amerekodi video yake ya wimbo wa kwanza wa ‘amani ya moyo’
‘My Papa’ ni single yake ya pili ambayo video yake kaifanya South Africa ambako ndio makazi yake kwa sasa, amekua akisoma pamoja na kufanya biashara kutumia jina lake.
Feza Kessy ni miongoni mwa mastaa wa Afrika ambao hulipwa zaidi ya shilingi milioni moja za Kitanzania kila anapotuma tweet moja kwenye page yake ya twitter akiisifia bidhaa au kampuni flani, ni biashara ambayo inafanyika sana kwa Afrika kusini.






0 maoni:
Chapisha Maoni