Jumapili, 7 Septemba 2014

MAKUBALIANO YA AMANI YAKIUKWA UKRAINE...


Mashambulizi nchini Ukraine

Milipuko mikali imesikika katika mji wa Bandari wa Mariupol mashariki mwa Ukraine.
Waandishi walioshuhudia makombora hayo wanasema kuwa kizuizi muhimu cha serikali kiliharibiwa na mashambulizi makali kutoka kwa wapiganaji wanaounga mkono Urusi.
Mji wa Mariupol unaonekana na wapiganaji wanaounga mkono Urusi kama muhimu katika barabara inayoelekea Crimea mbali na kuwa kitega uchumi cha eneo la Donbas iwapo litakuwa huru.
Mwandishi wa BBC katika mji huo amesema kuwa haijulikani iwapo mashambulizi hayo ni ya mda ama ni mwisho wa makubaliano ya kusitisha vita yalioafikiwa siku ya ijumaa.
Awali viongozi wa Urusi na Ukraine walisema kuwa wameridhika kuwa makubaliano hayo yanaafikiwa.
Rais Vladmir Putin na mwenzake wa Ukraine Petro Porishenko walizungumza kuhusu mwafaka huo kupitia njia ya simu.
Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limesema kuwa makombora yaliyalazimu malori ya misaada yaliokuwa yakielekea katika mji unaodhibitiwa na waasi wa Luhansk kurudi.
Share:

0 maoni:

MATUKIO YA VIDEO

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text