Ijumaa, 26 Septemba 2014

RAIS KIKWETE AKIKASIRIKA AU MTU AKIMUUDHI NYUMBAN HUWA ANAKUWA HIVI


JKLabda inawezekana hii ikawa mara yetu ya kwanza kusikia upande wa pili wa President wetu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ambae tumezoea tu kumuona akihutubia, akijumuika na watu mbalimbali kwenye matukio ya furaha na huzuni lakini kuna mengine hatuyajui kuhusu yeye.
Mtoto wake Ridhiwani Kikwete ambae ni mbunge wa Chalinze ameongea kwenyeExclusive na millardayo.com na kueleza ni jinsi gani inavyokua pale ambapo baba yake anakasirika au anapokasirishwa akiwa nyumbani.
Ridhiwani>>> ‘Jambo akiwa halitaki mara nyingi hupenda kusema achana na hilo lakini kama ni mtu kafanya jambo flani sio zuri utamsikia mzee tu anasema huyu mtu bwana achana nae….. maarifa yake madogo, naweza kutoa ushuhuda mbele za watu mzee wangu mimi sio mtu ambae ameishi kwenye mazingira yanayotoa fursa ya matumizi ya lugha ngumungumu kama matusi
Yani mtu akimuudhi… huwezi kusikia amefikia hatua ya kutamka labda huyu mshenziiii…. sina kumbukumbu ya mimi kumsikia akitamka neno kama hilo, mara nyingi ukikosea anasema huyu maarifa yake madogo kwelikweli‘ – Ridhiwani

chanzo cha audio: Millardayo.com


Share:

0 maoni:

MATUKIO YA VIDEO

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text