Jumatano, 17 Septemba 2014

VURUGU ZATOKEA HUKO MPAKANI MWA UGANDA NA SUDAN.......


Uganda 5Ripota wa TZA nchini Uganda Bill the African ameripoti kuhusu hii ya vurugu kubwa kutokea kwenye mpaka wa Uganda na Sudan eneo la Ufoju kutokana na raia wa nchi hizi mbili kutoafikiana kwenye baadhi ya mambo ambapo pia baadhi ya viongozi wa Uganda kwenye eneo hilo walikamatwa na Polisi wa Sudan.
Kikubwa kinachosababisha vurugu hizi ni mipaka ya hizi nchi kushindwa kujulikana kila mmoja anatakiwa kuishia wapi ambapo pia Waganda ambao wamekua wakiingia Sudan wamekua wakikamatwa na Polisi wa Sudan na kupewa mateso makubwa.
Uganda 4Jeshi la Polisi Uganda limesema kwamba katika vurugu hizi karibu nyumba 15 za raia wa Sudan wanaoishi Uganda zimechomwa moto likiwemo kanisa la kipentekoste linalodaiwa kuwa la raia wa Sudan.
Uganda 3
Uganda 1
Uganda 2
Pia waweza sikiliza hapa chini kupitia mtaarishaji wetu mahiri kabisa millardayo.com


Share:

0 maoni:

MATUKIO YA VIDEO

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text