
Yafuatayo ndio ameyasema:
- ‘Leo nitasema neno zito kidogo, litabadilisha sura ya historia yangu milele… kinachotokea hapa kina maana kubwa sana kwa watu wenye historia inayofanana na mimi, wale ambao wameyajua maisha ya shida na kukosa uhakika toka wakiwa tumboni mwa wazazi kutokana na hali za uchumi wa familia zao’
- ‘Nimeyajua maisha ya mtu mnyonge na masikini kwa kuyaishi na sio kwa kusoma ama kusikia, ninajua mtu akiongelea njaa anamaanisha nini’
3.’Watanzania wanataka kupata huduma bora za afya, elimu, maji, miundombinu…… ukienda kwa Wafanyabiashara wakubwa pale Pugu viwandani ama kwa Matabibu wenzangu hospitali ya taifa Muhimbili au kwa Wafanyabiashara pale sokoni Kariakoo wote watakwambia hawapendi kuona kodi zao zikitafunwa na wachache wasio waadilifu’
4.’Watu hawatarajii serikali itabeba mizigo yao yote lakini wanaamini kabisa kwamba tukibadili vipaumbele vyetu, tukibadili namna tunavyoendesha serikali na uchumi wetu, tunaweza kwa kiasi kikubwa kubadili mwelekeo mzima wa maisha ya baadae na kuiondoa Tanzania miongoni mwa nchi masikini kabisa duniani’
- ‘Na mimi kama Watanzania wenzangu wengi nina imani kubwa kabisa kwamba tunaweza kubadili mustakabali wa taifa letu, kufungua milango ya maisha bora zaidi kwa Watanzania, tutatoa fursa sawa kwa kila Mtanzania kuishi kwa matumaini kwamba atabadili maisha yake wakati wowote ule kuanzia leo, tutaweza kuamsha ari ya kila Mtanzania kuongeza bidii kwenye kazi’
‘Ninaamini kabisa kutokea ndani ya mifupa yangu kuwa tukifanya uchaguzi sahihi wa vipaumbele vyetu, tukibadili namna tunavyoendesha uchumi wetu na serikali yetu……. haya ninayoyasema sio ndoto za mchana’

JIBU: ‘Nitapitia chama cha mapinduzi, sijawahi kuwa Mwanachama wa chama chochote kile cha siasa zaidi ya CCM na sijawa na fikra za kubadili chama, natangaza nia ya kugombea Urais kupitia chama changu cha CCM, hii ya kwamba sasa hivi ni mapema mno kutangaza nia kwa sababu vyama havijafungua milango ya watu kutangaza nia, sio kweli…. watu wameweka nia za kuutaka Urais toka mwaka 1995 lakini pia kuweka nia sio kufanya kampeni, kinachokatazwa ni kuanza kufanya kampeni kabla ya muda wa kampeni kutangazwa’ – Dr. Hamisi Kigwangalla
‘Nimeamua kuweka wazi nia yangu, sitaki ule unafiki wa kujificha chini ya kivuli cha Ooooh!!….. nimeshauriwa, nimeombwa, nasubiri kuota, mimi ni mkweli na nimetia nia ya dhati kwamba nataka Urais’ – Dr. Kigwangalla


Dr. Hamis akilishwa keki yenye ramani ya Tanzania na mke wake kumalizia shughuli hii ya kutangaza nia
Unaweza kumsikiliza Dr. Kigwangalla kwenye dakika zake tisa hapa chini akijibu maswali.
0 maoni:
Chapisha Maoni