Jumatatu, 1 Septemba 2014

PICHA 7 ZILIZOTOKEA BAADA YA DIAMOND KUPELEKWA KWENYE SHOW SAA KUMI ALFA JIRI HUKO UJERUMANI


Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.38 AMMmiliki wa hit single ya ‘mdogo mdogo’ Diamond Platnumz anahusika tena kwenye zile habari zinazoongelewa sana ambapo time hii imetokea Stuttgart Ujerumani.
Alitakiwa kufanya show weekend iliyoisha sehemu inaitwa Stuttgart lakini ikashindikana baada ya kudai kucheleweshwa na Promota na badala yake akampeleka kwenye ukumbi saa kumi alfajiri.
Inasemekana mashabiki wenye hasira waliosubiri kuanzia saa nne usiku walianza kufanya fujo kwa kurusha chupa na kuvunja vyombo vya muziki vilivyokua vimefungwa hapo kwa madai pia kwamba vilikua vibovu ambapo inataarifiwa kwamba Ma Dj wawili walijeruhiwa kwa kiasi kikubwa pamoja na vyombo vyao kuharibiwa.
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.29 AMDiamond alipowasili saa kumi alfajiri tayari mashabiki walikua wametoka nje kama hivi ambapo mmoja wa mashabiki waliokuwemo kwenye tukio hilo amesema Polisi walilazimika kuingilia kati na Diamond hakudhurika.
Platnumz ambae ameahidi kuongea na Amplifaya ya CloudsFM aliandika kwenye mitandao yake ya kijamii muda mfupi baada ya hilo tukio >>>>‘kiukweli nimesikitishwa sana na uandaaji wa kampuni hii ya BRITTS EVENTS iliyoandaa show ya Stuttgart Germany, Promoter anatupeleka kwenye show saa kumi alfajiri
Naomba mtambue halikua kosa langu, mimi ni mgeni tu na ninafata maelekezo ya Promoter hivyo nisingeweza kujiamulia kuja muda ninaotaka mimi‘ – Diamond
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.12 AM
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.04 AM
Screen Shot 2014-09-01 at 12.15.56 AM
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.49 AM
Screen Shot 2014-09-01 at 12.16.59 AMPicha zimepigwa na OldMombasa
Share:

0 maoni:

MATUKIO YA VIDEO

Kumbukumbu la Blogu

Recent Posts

Unordered List

Pages

Theme Support

Sample Text